Vietnam imesitisha
shughuli ya uchimbaji gesi katika eneo linalozozaniwa kusini mwa bahari
ya China, kufuatia vitisho vikali kutoka China.
Ripoti zinasema kuwa wakurugenzi wa Respol waliambiwa wiki iliyopita na serikali wa Viertman kuwa China ilikuwa imetisha kushambulia vituo vyake katika visiwa vya Spratly ikiwa uchimbaji huo haungesitishwa.
China inadai kuwa karibu eneo lote la kusini mwa bahari ya China ni lake, visiwa ambavyo pia vinavyodaiwa na mataifa mengine.
Vietnam inaliita eneo hilo Block 136-03 na imeipa zabuni kampuni inayoitwa Talisman-Vietnam. China nayo inaliita eneo hilo Wanan Bei-21 ikiwa imetoa kandarasi kwa kampuni tofauti.
SHARE
No comments:
Post a Comment