Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO
la Soka Afrika (CAF), limewateua waamuzi wa Uganda kuchezesha mchezo wa
marudiano kati ya Amavubi ya Rwanda na Taifa Stars ya Tanzania. Katika
mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza timu hizo
zilitoka sare ya 1-1.
Mchezo
huo utakaofanyika Uwanja wa Nyamirambo, Jumamosi saa 10.00 jioni kwa
saa za Rwanda sawa na saa 9.00 alasiri kwa saa za Tanzania, utachezeshwa
na Brian Nsubuga Miiro ambaye atakuwa na jukumu la kupiliza kipenga.
Waamuzi
wasaidizi watakuwa Ronald Katenya (Line 1) na Dick Okello (Line 2)
wakati Mwamuzi wa akiba atakuwa Chelanget Ali Sabila huku Kamishna wa
mchezo atakuwa Ali Mohamed Ahmed kutoka Somalia.
Mchezo
huo ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN). Timu hiyo kwa mwaka huu
imecheza mechi 10 za kimataifa na kushinda mitano; kutoka sare minne na
kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa.
Wakati
huoh huo: Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa
Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA), Ramadhani Mambosasa ametangaza majina
manane ya wagombea waliopitishwa katika usaili katika mchakato uchaguzi
unaotarajiwa kufanyika Agosti 10, mwaka huu mjini Dodoma.
Waliopitishwa
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi - ngazi ya taifa ni pamoja na
Kidao Wilfred, Lisiter Manyara, Michael Bundala, Dismas Haonga, Jamhuri
Kihwelo, George Komba, Samuel Moja na Mwalwasi.
Nafasi
zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu
Msaidizi, Mweka Hazina, Wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati
ya Utendaji.
SHARE
No comments:
Post a Comment