Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WINGA
wa Yanga SC, Simon Msuva atakwenda Morocco wiki ijayo kufanya vipimo
vya afya katika mpango wa kujiunga na klabu ya Ligi Kuu nchini humo,
Difaa Hassani El-Jadida kwa ada ya uhamisho ya dola za Kimarekani
150,000 zaidi ya Sh Milioni 300 za Tanzania.
Difaa
ambayo tayari imekwishamchukua Mtanzania mwingine, winga pia Ramadhani
Singano ‘Messi’ kutoka Azam FC iko tayari kutoa dola 150,000 kumnunua
Msuva ambaye amebakiza miezi tisa katika mkataba wake Yanga.
Msuva
alishindwa kuondoka jana kwenda Kigali, Rwanda na kikosi cha timu ya
taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya kwanza
kuwania tiketi ya Faianli za Ubingwa wa Mataifa wa Afrika (CHAN),
zinazohusisha wachezaji wanaocheza nchini mwao pekee, ili kushughulikia
safari yake Morocco.
Simon
Msuva atakwenda Morocco wiki ijayo kufanya vipimo vya afya kuelekea
uhamisho wake wa dola 150,000 kwenda Difaa Hassani El-Jadida
Na baada ya kukamilisha taratibu zote, Msuva ameondoka Dar es Salaam kwenda Kigali kuungana na Stars kujaribu kupata matokeo mazuri ugenini baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Mwanza Jumamosi.
Na baada ya kukamilisha taratibu zote, Msuva ameondoka Dar es Salaam kwenda Kigali kuungana na Stars kujaribu kupata matokeo mazuri ugenini baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Mwanza Jumamosi.
Baada
ya mchezo na Amavubi mjini Kigali Jumamosi, Msuva aliyejiunga na Yanga
mwaka 2012 kutoka Moro United, anatarajiwa kwenda moja kwa moja Morocco
kwa ajili ya vipimo vya afya ambavyo akifuzu atasaini mkataba mnono.
Timu
hiyo yenye maskani yake mji wa El Jadida ikiwa inatumia Uwanja wa El
Abdi inataka kujaribu kutwaa taji la Ligi Kuu ya Morocco, inayojulikana
kama Botola, moja ya Ligi bora kabisa barani Afrika.
SHARE
No comments:
Post a Comment