Ikiwa
ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kila
mtoto kuanzia chekechekea mpaka kidato cha nne wanapata elimu bure,
kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania leo imetoa vitabu vya sayansi
kwa shule za mkoa wa Sumbawanga vyenye thamani ya shilingi milioni kumi
TZS 10,000,000. Vitabu hivyo vimepokelewa na Mbunge wa Jimbo la kalambo
Mh, Josephat Kandege na kugaiwa kwa shule zenye uhabu wa vitabu jimboni
humo.
Akiongea
wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Mbunge wa Jimbo la kalambo Mh,
Josephat Kandege alisema “ muhimu kutambua mchango wa makampuni binafsi
kama Airtel Tanzania kwa juhudi za dhati za kuunga mkononi serikali yetu
katika kuninua sekta ya elimu hapa nchini. sote tunajua ya kwamba
serikali yetu inaongozwa na sera ya serikali ya viwanda. Kwa maana hiyo
hatuwezi kuwa na viwanda bila ya kuwa na wanasayansi, hiyo basi vitabu
hivi vitaongeza chachu kwa wanafunzi wetu wa kuendelea kufanya vizuri
katika masomo ya sayansi na hatimaye kufanikisha ndoto zao pamoja na
serikali”.
Mh
Kandege aliendelea kusema kwamba “nawaomba Airtel na wadau wengine
waendelee kutusaidia kwenye nyaja zingine mbali mbali ili kuendelea
kutengeneza mazingira bora kwa wanafunzi kujifunza na hivyo kuongeza
uelewa na kuwa na taifa lenye ueledi”.
Kwa
upande wake Meneja Mauzo wa Airtel Rukwa na Katavi Bw, Hapson Kamanya
alisema “Airtel tunaamini jamii iliyoelimika inajengwa kutoka katika
shule zenye vifaa vya kufundishia vya kutosha hususani vitabu, ili kuwa
na maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo
tunathibitisha dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu katika shule
hizi”.
Tunaamini
ya kwamba msaada wa vitabu utachochea ufaulu mzuri katika masomo ya
sayansi katika mkoa na pia utaongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma
masomo ya sayansi” Aliongeza Kamenya.
Kwa
upande Mkuu wa shule ya Mwazye Bw, Haron Mwaibabu akiongea kwa niaba ya
shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivyo alisema “Msaada huu
umekuja wakati muafaka wakati shule zetu zimekuwa na upungufu wa vitabu
na tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo".
Aliongeza,
ni ukweli kuwa shule zetu zina uhaba wa vitabu vya sayansi kitu ambacho
kilikuwa kinatupa ugumu kwenye kufundisha na hata kupelekea baadhi ya
wanafunzi wetu kutotamani kuchukua masomo ya sayansi. Tunashukuru sana
Airtel kwa kuwa mkombozi kwenye hili’.
Diwani
wa Kata ya Mambo Nkose Kanowalya Siwale (kushoto), Meneja Mauzo Airtel
Tanzania Kanda ya Rukwa Hudson Kamenya (wa pili kushoto), Jimbo la
Kalambo mkoani Sumbawanga Josephat Kandege wakimkabidhi vitabu vya
sayansi Makamu wa shule ya Sekondari ya Kalambe Charles Mnkonya (kulia).
Vitabu hivyo vyenye thamani ya TZS10,000,000 vimetolewa na Airtel
Tanzania kwa shule za sekondari zenye uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye
Jimbo la Kalambo.
Wanafunzi
wa shule ya sekondari ya Kalembe wakiwa kwenye picha ya pamoja na
Meneja Mauzo Airtel Tanzania kanda ya Rukwa Hudson Kamenya baada ya
kampuni ya Airtel Tanzania kukabidhi vitabu vya sayansi vyenye thamani
ya Tzs10,000,000/- mwishoni mwa wiki kwa jimbo la Kalambo mkoani
Sumbawanga.
Meneja
Mauzo Airtel Tanzania kanda ya Rukwa Hudson Kamenya (katikati) na
Mbunge wa Jimbo la Kalambo mkoani Sumbawanga wakimkabidhi Mwalimu wa
somo la Kemia kwenye shule ya sekondari ya Mwazye Aidin Mwaibabu baadhi
ya vitabu vilivyotolewa na kampuni ya Airtel Tanzania kwa shule za
sekondari zenye uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye Jimbo la Kalambo.
SHARE
No comments:
Post a Comment