NA K-VIS
BLOG.MASHIRIKA YA HABARI
MWENYEKITI wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini
Kenya, (IEBC) Wafula Chebukati amemtangaza Rais
aliye madakani nchini humo, Bw. Uhuru Kenyatta, kuwa mshindi wa kiti cha Rais
wa nchi hiyo kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 8, 2017, licha ya
malalamiko ya upande wa upinzani kuwa tume isitangaze matokeo hayo hadi hapo
watakapolinganisha matokeo yaliyokuwa yanakusanywa na mawakala wao nay ale ya
tume.
![]() |
| Bw. Odinga |
Kwa mujibu wa Mwenyejkiti wa tume hiyo, Rais Kenyatta
ambaye alikuwa anawania muhula wake wa pili na wa mwisho chini ya nmwamvuli wa
vuguvugu la Jubilee, alipata asilimia 54.27 ya kura zilizopigwa, huku hasimu
wake mkuu, Bw. Raila Odinga wa vuguvugu la NASA, akiambulia asilimia 44.74 ya
kura zilizopigwa.
Kwa mujibu wa sheria za uchanguzi nchini Kenya,
mshindi pia anatakiwa apate asilimia 25 ya kura kwa uchache kutoka nusu ya
kaunti zote 47 zinazounda Jamhuri ya Watu wa Kenya.
Zaidi ya Wakenya Milioni 15 walipiga kura kwenye
uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali baina ya Bw,. Kenyatta na Bw. Odinga mwenye
umri wa miaka 72 amewania nafasi hiyo kwa mara ya nne bila mafanikio.
Rais Kenyatta na Makamu wake William Ruto, (pichani juu), sasa
wataendelea kusalia madarakani na hivyo kuhakikisha ahadi walizowapatia Wakenya
wanazikamilisha.
Wawili hao wanasifika kwa umahiri wao wa kujieleza
mbele ya wapiga kura na wachambuzi wa masuala ya siasa hapa Tanzanai,
wanawafananisha na “Boys II Men” wanamuziki wa zamani wa Marekani waliojizolea
umaarufu mkubwa miongoni mwa wapenzi wa muziki.
Lakini pia historia ya wawili hao inaonyesha
mshikamano wao hata pale wanapokabiliana na matatizo kama ile kesi ya
kihistoria ya ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo Wakenya
wanaofikia 1000 waliuawa ambapo Kenyatta na Ruto, walishtakiwa kwenye mahakama
ya kimataifa ya makosa ya jinai kabla ya mahakama hiyo kuwafutia mashtaka kwa
kukosekana kwa ushahidi wa kutosha. tayari Rais Dkt. John Pombe Magufuli ame-tweet kumpongeza Rais mteule wa Kenya Bw. Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa tena kuiongoza Kenya.
Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya, (IEBC), Bw. Wafula Chabukati, akitangaza matokeo Agosti 11, 2017.
Wafuasi wa Jubilee wakishanglia ushindi
Mkuu wa mkakati wa Vuguvugu la muungano wa NASA, David Ndii na Bela Akinyi wakihutubia
mkutano na waandishi wa habari kwenye ngome yao ya Rundo, wakituhumu “uchakachuaji”
wa matokeo ya uchaguzi wa Urais.
SHARE













No comments:
Post a Comment