Mke wa rais wa
Zimbabwe Robert Mugabe, Grace Mugabe, ambaye anaomba kinga ya
kidiplomasia kufuatia madai ya kumshambulia mwanamitindo, anatarajiwa
kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kikanda Afrika kusini baadaye leo.
Serikali ya Afrika kusini imekanusha madai kwamba ilipania kumkabidhi Bi. Grace Mugabe kinga ya kidplomasia baada ya kutuma ombi lake.
Polisi wameweka ulinzi mkali kwenye mipaka ya taifa hilo kuhakikisha kwamba Bi. mugabe hatotoroka.
- Afrika kusini yaweka 'tahadhari' mipakani kumzuia Bi Mugabe
- Mke wa Mugabe akosa kufika mahakamani Afrika Kusini
Engels aliambia BBC kwamba alishambuliwa na bi Mugabe aliyeamini kwamba alikuwa akijua kule aliko mwanawe Bellarmine.
''Tuliendelea kumwambia hatujui aliko...hatujamuona usiku wote...alinikamata na kuanza kunipiga.Nakumbuka nikianguka katika sakafu na damu nyingi katika uso na shingo yangu.Alitupiga akiwa na chuki nyingi'', alisema msichana huyo.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment