Kamishna wa Madini Tanzania,
Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mbele), Kamishna Msaidizi wa Nishati
anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile (wa kwanza kulia
mstari wa mbele) ambaye ameeleza kuhusu uwekezaji katika masuala ya
umeme kwa kutumia makaa ya mawe. Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 18
Agosti, 2017 katika ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es
Salaam. Wengine katika picha ni wajumbe kutoka Taasisi zilizo chini ya
Wizara.
Kamishna wa Madini Tanzania,
Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mbele) akieleza jambo mbele ya wajumbe
walioshiriki kikao baina ya Wizara na Wawekezaji wa Kampuni ya
Hyundai E & C.
Wajumbe kutoka Wizara ya Nishati
na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Madini ya Taifa (STAMICO) na Wakala
wa Nishati Vijijini (REA) wakifatilia mada katika kikao baina ya Wizara
na Kampuni ya Hyundai E & C.
Kamishna wa Biashara nchini kutoka
Ubalozi wa Korea, Jeon, Heesu (anayetoa maelezo) akielezea uzoefu wa
Kampuni ya E & C katika masuala ya Nishati katika kikao
kilichofanyika Wizara ya Nishati. Wengine katika picha ni Ujumbe kutoka
Kampuni ya Hyundai E & C pamoja na Wawakilisha kutoka Benki ya Exim
nchini.
……………….
Na Rhoda James
Wizara ya Nishati na Madini
imekutana na Kampuni ya Hyundai E & C ya Korea Kusini ambayo
imeonesha nia ya kuwekeza katika vyanzo vipya vya nishati nchini.
Kampuni hiyo na Wizara wamekutana
jijini Dar es Salaam ambapo kikao hicho pia kimehudhuriwa na taasisi
zilizo chini ya Wizara likiwemo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Madini ya
Taifa (STAMICO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Akizungumzia kuhusu uwekezaji
huo, Kamishna wa Nishati anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James
Andilile amesema kuwa Serikali inakaribisha wawekezaji zaidi kuwekeza
nchini hususan katika vyanzo vipya vya umeme ikiwemo Makaa ya Mawe,
miradi inayotumia nguvu za maji, pamoja na miradi ambayo bado haijaanza
kutekelezwa.
Andilile ameeleza kuhusu miradi
mikubwa ya nishati inayoendelea kutekelezwa nchini kwa sasa ikiwemo ile
ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia na kuitaja kuwa ni pamoja na
Mradi wa Kinyerezi II wa Megawati 240, Kinyerezi I Extension Megawati
185.
“Ipo miradi ambayo inahitaji
ufadhili au Serikali inahitaji kuingia ubia na Kampuni za ndani na nje
ili kuifanikisha, mojawapo wa miradi hiyo ni Kiwira ambao Serikali
ingependa kuona unaanza haraka,” amesisitiza Andilile.
Kwa upande wake Mwakilishi wa
Kampuni ya Hyundai E & C, Dongil Chang amesema kuwa, kampuni hiyo
inayo nia ya kuwekeza Tanzania kwa kuwa inao uzoefu mkubwa katika
masuala ya Nishati.
Ameongeza kuwa, kampuni hiyo ni ya 13 kwa ukubwa Duniani hivyo inavyo vigezo na uwezo wa kutekeleza miradi mbalimbali.
“Tupo tayari kuwekeza Tanzania
katika sekta ya Nishati. Mara baada ya kupata taarifa zote muhimu kwa
ajili ya uwekezaji bila shaka tutaanza majadiliano mara moja.” ameongeza
Chang.
SHARE
No comments:
Post a Comment