![2](http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/08/2-46.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Zanzibar
jioni ya leo tayari kuhudhuria sherehe ya Siku ya Kizimkazi
itakayoadhimishwa kesho tarehe 12 Agosti, 2017.
Akiwa katika Uwanja
wa Ndege wa Abeid Karume, Makamu wa Rais amekutana na Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland ambaye alikuwa safarini kuelekea
Dar es Salaam akiwa ameongozana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza
Dk. Asha-Rose Migiro.
Bi. Scotland alikuwa
mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
SHARE
No comments:
Post a Comment