Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Anne Makinda akisaini
kitabu cha wageni kwenye banda la NHIF jijini Dodoma
alipotembelea maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya
Nzuguni jijini humo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw.
Bernard Konga na viongozi wengine wa NHIF wakimsikiliza kwa makini
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF alipotembelea banda hilo Jijini Dodoma kwenye
maonesho ya Nanenane.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Mhe. Anne Makinda
akisalimiana na mmoja wa maofisa wa NHIF waliokua wakishiriki maonesho
ya Nanenane Jijini Dodoma.
Meneja wa NHIF mkoani Dodoma Bi. Salome Manyama akielezea jambo
kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Mhe. Anne Makinda ambaye
pia alitembelea banda hilo kama mgeni Rasmi wa maonesho hayo ya
Nanenane yaliyokua yakifanyika jijini Dodoma kwenye viwanja vya
Nzuguni.
……………………………
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF
Mhe. Anne Makinda ametembelea Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya
Nzuguni Mjini Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi wa siku hiyo. Mhe.
Makinda alisisitiza umuhimu wa kila mtanzania kuwa na bima ya afya ili
kuwa na uhakika wa matibabu na kuweza kutimiza majukumu yake ya kila
siku na kuepukana na umaskini.
Alisema ‘…. tunajua kuwa katika
zama hizi tunatakiwa kuchapa kazi kama Mhe. Rais wetu anavyotuhimiza,
lakini ili tuweze kuendana na kasi hii hatuna budi kuwa na uhakika na
afya zetu na Serikali imetuletea utaratibu huu wa bima ya afya ambao ni
rahisi kwa kila mtu kujiunga na kuwa na uhakika wa matibabu pindi
anapougua”
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga amesema NHIF imejipanga kutoka na kwenda
kuwafuata watu walipo ili kuweza kuwasajili na huduma za Mfuko huo.
Alisema kwa sasa Mfuko unafanya kampeni ya uhamasishaji wa huduma ya
bima ya afya kwa watoto walio chini ya miaka 18 ijulikanayo kama TOTO
AFYA KADI. “Mfuko umeanza kufanya usajili kwa wingi katika maeneo
mbalimbali karibu na watu walipo ambapo kila mtoto anachangiwa sh.
50,400 tu kwa mwaka” alisema Bw. Konga.
Huduma hii ya TOTO AFYA KADI
imezinduliwa rasmi na Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wiki iliyopita ambaye alisema kuwa watoto
ambao ni asilimia 51 ya watanzania wote wanahitaji kuwa na uhakika wa
matibabu na alihimiza kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha watoto hawa
wanapata huduma hiyo.
Naye Meneja wa NHIF Mkoani Dodoma,
Bi. Salome Manyama amesema wazazi na walezi wamepata mwitikio na kufika
kusajili watoto wao katika huduma ya TOTO AFYA KADI katika maonesho
hayo. Ameongeza kusema kuwa umma uko tayari na wamejipanga kuendeleza
kampeni hiyo katika maeneo ya karibu zaidi na wananchi.
SHARE
No comments:
Post a Comment