Korea Kaskazini imedokeza kwamba
inatafakari uwezekano wa kurusha makombora karibu na jimbo la Marekani
la Guam katika bahari ya Pasifiki, saa chache baada ya Rais wa Marekani
Donald Trump kuitishia Pyongyang kwamba itakabiliwa kwa "moto na
ghadhabu".

Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini
limesema taifa hilo linatafakari mpango wa kurusha makombora ya masafa
ya kati na mbali karibu na Guam, eneo ambalo Marekani huwa na ndege zake
za kuangusha mabomu.Taarifa hiyo inaashiria kuongezeka kwa uhasama kati ya nchi hizo mbili.
Umoja wa Mataifa hivi majuzi uliidhinisha vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo.
Rais Trump ametoa tamko lake baada ya ripoti kwenye vyombo vya habari kusema kwamba Korea Kaskazini imeweza kuunda kichwa cha silaha za nyuklia chenye uwezo wa kutosha kwenye makombora yake.
- Trump: Tutaikabili Korea Kaskazini kivita ikiendelea na vitisho
- Trump: Ningependa kukutana na Kim Jong-un
Taarifa ya gazeti la Washington Post, ikunukuu maafisa wa ujasusi wa Marekani, imedokeza kwamba Korea Kaskazini inaunda silaha za nyuklia zenye uwezo wa kuishambulia Marekani kwa kasi zaidi ya iliyotarajiwa.
Shirika la habari la Korea Kaskazini (KCNA) limesema jeshi la nchi hiyo "linachunguza kwa makini mpango wa kuanzisha moto wa kuzingira Guam kwa kutumia makombora ya roketi ya masafa ya wastani na ya masafa marefu ya Hwasong-12".
Shirika hilo limesema mpango huo utawasilishwa kwa Viongozi Wakuu baada ya "kutathminiwa kwa kina na kukamilishwa" na utatekelezwa kiongozi wake Kim Jong-un akiamrisha, shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap limeripoti.
Kisiwa muhimu cha Guam
- Kisiwa cha Guam kina ukubwa wa kilomita mraba 541 (maili mraba 209) na kinapatikana bahari ya Pasifiki kati ya Ufilipino na Hawaii.
- Ni jimbo "lisilo na mpangilio wowote, na lisilojumuishwa kikamilifu" la Marekani, lenye wakazi karibu 163,000.
- Kambi za jeshi la Marekani hutumia karibu robo ya ardhi ya kisiwa hicho. Marekani ina wanajeshi 6,000 kisiwa hicho na kuna mipango ya kuwasafirisha maelfu wengine huko.
- Ni kituo muhimu katika shughuli za kijeshi za Marekani, ambapo huwezesha wanajeshi wa nchi hiyo kufika maeneo mengi muhimu Pasifiki, mfano eneo la bahari linalozozaniwa la South China Sea, rasi ya Korea na mlango wa bahari wa Taiwan.
Bw Trump aliambia wanahabari Jumanne kwamba: "Korea Kaskazini wasidhubutu kutoa vitisho zaidi kwa Marekani. Watajibiwa kwa moto na ghadhabu ambayo ulimwengu haujawahi kushuhudia."
Seneta mkongwe wa Marekani John McCain hata hivyo alikuwa na shaka kuhusu tamko la Trump.
"Viongozi wengi wakuu ambao nimewahi kuwaona, huwa hawatoi vitisho ikiwa hawako tayari kuvitekeleza na sina uhakika kwamba Rais Trump yuko tayari kuchukua hatua," alisema Bw McCain.
Korea Kaskazini ilikuwa imeghadhabishwa na vikwazo vipya ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi.
Vikwazo hivyo vina lengo la kupunguza mapato kutoka kwa mauzo ya bidhaa nje ya Korea Kaskazini kwa theluthi moja.
KCNA imesema Korea Kaskazini, ambayo imefanyia majaribio silaha za nyuklia mara tano, itajibu vikali na kwamba "Marekani italipia" kwa kuchangia kutunga vikwazo hivyo.
Taarifa hiyo inaashiria kuongezeka kwa uhasama kati ya nchi hizo mbili. Umoja wa Mataifa hivi majuzi uliidhinisha vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo.
Rais Trump ametoa tamko lake baada ya ripoti kwenye vyombo vya habari kusema kwamba Korea Kaskazini imeweza kuunda kichwa cha silaha za nyuklia chenye uwezo wa kutosha kwenye makombora yake.
- Trump: Tutaikabili Korea Kaskazini kivita ikiendelea na vitisho
- Trump: Ningependa kukutana na Kim Jong-un
Taarifa ya gazeti la Washington Post, ikunukuu maafisa wa ujasusi wa Marekani, imedokeza kwamba Korea Kaskazini inaunda silaha za nyuklia zenye uwezo wa kuishambulia Marekani kwa kasi zaidi ya iliyotarajiwa.
Shirika la habari la Korea Kaskazini (KCNA) limesema jeshi la nchi hiyo "linachunguza kwa makini mpango wa kuanzisha moto wa kuzingira Guam kwa kutumia makombora ya roketi ya masafa ya wastani na ya masafa marefu ya Hwasong-12".
Shirika hilo limesema mpango huo utawasilishwa kwa Viongozi Wakuu baada ya "kutathminiwa kwa kina na kukamilishwa" na utatekelezwa kiongozi wake Kim Jong-un akiamrisha, shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap limeripoti.
Kisiwa muhimu cha Guam
- Kisiwa cha Guam kina ukubwa wa kilomita mraba 541 (maili mraba 209) na kinapatikana bahari ya Pasifiki kati ya Ufilipino na Hawaii.
- Ni jimbo "lisilo na mpangilio wowote, na lisilojumuishwa kikamilifu" la Marekani, lenye wakazi karibu 163,000.
- Kambi za jeshi la Marekani hutumia karibu robo ya ardhi ya kisiwa hicho. Marekani ina wanajeshi 6,000 kisiwa hicho na kuna mipango ya kuwasafirisha maelfu wengine huko.
- Ni kituo muhimu katika shughuli za kijeshi za Marekani, ambapo huwezesha wanajeshi wa nchi hiyo kufika maeneo mengi muhimu Pasifiki, mfano eneo la bahari linalozozaniwa la South China Sea, rasi ya Korea na mlango wa bahari wa Taiwan.
Trump aliambia wanahabari Jumanne kwamba: "Korea Kaskazini wasidhubutu kutoa vitisho zaidi kwa Marekani. Watajibiwa kwa moto na ghadhabu ambayo ulimwengu haujawahi kushuhudia."
Seneta mkongwe wa Marekani John McCain hata hivyo alikuwa na shaka kuhusu tamko la Trump.
"Viongozi wengi wakuu ambao nimewahi kuwaona, huwa hawatoi vitisho ikiwa hawako tayari kuvitekeleza na sina uhakika kwamba Rais Trump yuko tayari kuchukua hatua," alisema Bw McCain.
Korea Kaskazini ilikuwa imeghadhabishwa na vikwazo vipya ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi.
Vikwazo hivyo vina lengo la kupunguza mapato kutoka kwa mauzo ya bidhaa nje ya Korea Kaskazini kwa theluthi moja.
KCNA imesema Korea Kaskazini, ambayo imefanyia majaribio silaha za nyuklia mara tano, itajibu vikali na kwamba "Marekani italipia" kwa kuchangia kutunga vikwazo hivyo.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment