Tume ya uchaguzi imetangaza matokeo kutoka kwa vituo 36659 kati ya jumla ya vituo 40883 ambapo:
- Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,461,933 (54.64%)
- Raila Odinga wa ODM kura 6,079,136 (44.51%)
- Joseph Nyagah (huru) 33,710 (0.25%)
- Abduba Dida wa ARK 29,411 (0.22%)
- Ekuru Aukot wa Thirdway Alliance 23,976 (0.18%)
- Japheth Kaluyu (huru) 10,316 (0.08%)
- Cyrus Jirongo wa UDP 10,019 (0.07%)
- Michael Wainaina (huru) 7,919 (0.06%)
Ili kushinda, mgombea urais anahitajika kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa, na angalau asilimia 25 katika kaunti 24 kati ya kaunti 47 nchini humo.
Iwapo hakuna mgombea atakayetimiza hilo, basi uchaguzi wa marudio utafanyika katika kipindi cha siku 30.Bw Kenyatta aliwahimiza Wakenya kudumisha umoja alipokuwa akipiga kura Jumanne
Kura zinaendelea kuhesabiwa na matokeo kutangazwa baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Kenya Jumanne.
Kenyatta aliwahimiza Wakenya kudumisha umoja alipokuwa akipiga kura Jumanne
Kura ambazo zilikuwa zimeharibika kufikia wakati huo ni 353,389.
Muungano wa Nasa umepinga matokeo yanayoendelea kutangazwa na tume hiyo na kusema si sahihi.
Bw Odinga amesema IEBC imefanya makosa kwa kutangaza matokeo hayo bila kuwaonyesha maajenti wa vyama Fomu 34A, kubainisha matokeo hayo yametoka katika vituo gani.
Katika baadhi ya vituo, shughuli ya upigaji kura ilichelewa kuanza na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) iliongeza muda kufikia wakati uliokuwa umepotezwa kabla ya kufungua vituo.
Kisheria, vituo vilitakiwa kufunguliwa saa kumi na mbili asubuhi na kufungwa saa kumi na moja jioni saa za Afrika Mashariki.
Lakini katika baadhi ya maeneo, mvua kubwa ilitatiza uchukuzi na upigaji kura na kwingine hitilafu za kimitambo zikachangia kukwamisha upigaji kura. Muda wa kufungwa kwa vituo uliongezwa kwa vituo vilivyochelewa kufunguliwa.
Wengi wanahofia uwezekano wa kutokea tena kwa ghasia za baada ya uchaguzi sawa na ilivyotokewa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Watu zaidi ya 1,100 walifariki na wengine 600,000 kuachwa bila makao.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment