Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amesema kuongezeka joto katika
betri za sola ndio chanzo cha moto uliounguza Nyumba ya Mbunge wa
Kigoma mjini, Zitto Kabwe juzi jioni.
Nyumba hiyo ipo mtaa wa Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga katika wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.
Amesema joto hilo limesababisha mlipuko wa moto kwenye betri za sola na hivyo nyumba kushika moto na kuteketea yote.
Polisi
wanamshikilia mlinzi wa nyumba hiyo, Norbert Joseph kwa mahojiano zaidi
ili kubaini kama kuna uzembe wowote uliofanywa na kusababisha moto
kuwaka.
Msaidizi
wa Zitto anayeifahamika kwa jina la Nyembo Mustafa ametaja thamani ya
hasara iliyosababishwa na moto huo kwamba ni Sh 45 milioni.
SHARE
No comments:
Post a Comment