Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia)
akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Utalii, kutembelea Mapango ya Amboni Jijini Tanga leo. Wengine pichani
ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Atashasta Ndetiye (wa pili kushoto),
Wajumbe wa kamati hiyo, Nape Nnauye (kushoto) na Shaban Shekilindi
(kulia).
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia
sehemu ya barabara iliyomeguka ndani ya eneo la Mapango ya Amboni.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii
wakipata maelezo ya vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya Mapango ya
Amboni kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Jumanne Gekora (kushoto).
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (wa pili
kulia) na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Utalii wakiangalia vivutio mbalimbali vya maumbo asilia
ikiwemo ya wanyama na alama za kuabudia vilivyomo ndani ya mapango hayo.
Muoneshaji
wa Kujitolea katika Mapango ya Amboni, Othman Mangula (kulia)
akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Utalii moja umbo la asili lenye taswira ya Chui ndani ya Mapango ya
Amboni ambapo ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii ndani ya
mapango hayo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mipango, Dkt. Iddi Mfunda (kulia) na Muwakilishi wa
Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Canisius
Karamaga (wa pili kulia) wakiangalia baadhi ya vivutio katika mapango ya
Amboni.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani na baadhi ya wajumbe wa msafara huo wakiwa ndani ya mapango ya Amboni.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani akipenya kwenye njia nyembamba iliyopo ndani ya mapango ya Amboni.
Moja ya umbile la asili lililojitengeneza ndani ya mapango ya Aamboni likiwa na taswira ya kwato za ngo'mbe.
Maumbo
mbalimbali ya asili yenye taswira ya viumbe ni moja ya kivutio kikubwa
ndani ya mapango ya Amboni, Pichani ni umbo la asili lenye taswira ya
matiti ambalo lipo ndani ya mapango hayo.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia)
akimsaidia Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bungu Ardhi, Maliasili na
Utalii, Neema Mgaya kushuka katika moja ya mteremko uliopo ndani ya
mapango hayo.
Muwakilishi
wa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii
Canisius Karamaga akifurahia jambo ndani maporomoko hayo.
Mkurugenzi
wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mtango
Mtahiko ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Alan Kijazi akiwa ndani
ya mapango hayo.
Picha na; Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii
SHARE
No comments:
Post a Comment