TRA

TRA

Wednesday, September 27, 2017

Kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya aliyekuwa mhasibu wa TRA yapigwa kalenda.

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabiki watu watatu akiwemo Mhasibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Reuben Mwakasa, umeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa shauli hilo bado haujakamilika.

washtakiwa hao ambao walifikishwa majakamani hapo wiki iliyopita na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia hasara TRA ya sh. bilioni 29.

Mbali na Mwakasa, mkazi wa Msagara, Moshi, Kilimanjaro, washitakiwa wengine ni Meneja wa Tema Enterprises, Ephraim Magete, mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na mfanyabiashara Elizabeth Massawe, mkazi wa Makongo Juu.

Mwendesha mashtaka wakili wa serikali mwandamizi Mutalemwa Kishenyi amedai mahakamani hapo kuwa kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haijakamilika.

Awali wakisomewa hati ya mashtaka na wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, ilidaiwa, kati ya Novemba 22, 2013 na Agosti 21, mwaka huu, katika maeneo mbalimbali wilaya za Temeke na Ilala.

washitakiwa hao kwa pamoja kwa vitendo vyao waliisababishia mamlaka hiyo hasara ya kiasi hicho kwa kukwepa kulipa kodi kwenye mamlaka hiyo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Octoba 11, mwaka huu.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger