
Hatimaye
ahadi ya shabiki wa Simba, ambaye ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed
Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji amekamilisha ahadi aliyoisema
kabla ya mkutano mkuu wa Simba kwa kukabidhi Milioni 100 kwa uongozi wa
Simba kwa ajili ya kufanya usajili.
MO
amekabidhi pesa hizo baada ya kueleza mipango yake kwa Simba ya kuwa
kama wanachama wa Simba wataridhia kufanya mabadiliko basi atachangia
pesa ya usajili jambo ambalo katika mkutano wake wa Jumatatu na
waandishi wa habari kuwa ahadi yake ni kweli na ataikamilisha kabla ya
dirisha la usajili kufungwa.
Akizungumza
baada ya kupokea cheki kutoka kwa MO, Rais wa Simba, Evans Aveva,
amemshukuru MO kwa msaada huo na sasa wanasimba watatembea kwa kujiamini
kwani wamepata pesa ya kufanya usajili.
“Nakushukuru
MO kwa msaada ambao umetupatia tunaamini ni mapenzi ambayo unayo kwa
Simba ndiyo umefanya uwe tayari kutoa pesa hizi na sisi tunaamini
zitaweza kutusaidia kupiga hatua na hata tuweze kutembea kifua mbele,”
alisema Aveva.
Aidha
Aveva alisema kiasi hicho cha pesa bado hakijatosha kwa kufanya usajili
ambao wamepanga kuufanya lakini kitawasaidia kupiga hatua ya kufanya
usajili ambapo kwa msimu huu wamepanga bajeti ya Milioni 400 lakini pia
kumtaja mchezaji wa Ivory Coast ambaye wanataka kumsajili ni Fredrick
Blagnon.
Kwa
uapnde wa MO alisema ametoa msaada huo kama sehemu ya ahadi aliyoitoa
kabla ya mkutano mkuu na hakuna makubaliano yoyote lakini pia kuwapa
ahadi mashabiki wa Simba kuwa kama akipata nafasi ataweka bajeti zaidi
ya Bilioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya usajili.
Chanzo Mo Blo (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment