TIMU
ya African Sports “Wanakimanumanu”imepata msaada wa vifaa vya michezo
kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi daraja la pili itakayoanza
kutimua vumbi.
Vifaa
hivyo ambavyo ni seti ya viatu vilitolewa juzi na Mbunge wa Jimbo la
Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku katika halfa iliyofanyika kwenye viwanja
wa CCM Mkwakwani mjini Tanga
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo,Mbunge Mussa alisema ameamua kutoa
vifaa hivyo ili kuweza kuihamasisha kufanya vizuri katika mashindano
hayo na hatimaye kuweza kurudi ilipotoka.Alisema licha ya timu hiyo kushuka daraja hivi sasa wanapaswa kujiimarisha na kucheza kwa umakini mkubwa ili kuweza kucheza michuano ya ngazi za juu.
“Mimi
ni Mbunge lakini pia ni mwana michezo hivyo nitahakikisha nazisapoti
timu za mkoa huu kwa lengo la kurejea kwenye makali yao ya zamani kwani
michezo ni ajira “Alisema.Nay
kwa upande wake,Mweka Hazina wa timu hiyo,Sad Juma alimshukuru mbunge
huyo kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia timu hiyo kuondokana na
uhaba uliokuwepo.
“Kama
unavyojua sisi tulikuwa na uhaba wa vifaa vya michezo hususani viatu na
nyenginevyo hivyo alichotupa mbunge tunamshukuru lakini tutakuwa nawe
bega kwa bega “Alisema.Hata
hivyo alisema hivi sasa wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya
kujiwinda na mashindano hayo wakiwa na kikosi imara ambacho kimedhamiria
kupata mafanikio.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi viatu Mweka Hazina wa timu ya African
Sports,Sad
Juma kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Ligi Daraja la pili
makabidhiano hayo yalifanyika uwanja wa CCM mkwakwani mjini Tanga
Mbunge
wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi viatu
Mweka Hazina wa timu ya African Sports,Sad Juma kwa ajili ya kujiandaa
na michuano ya Ligi Daraja la pili makabidhiano hayo yalifanyika uwanja
wa CCM mkwakwani mjini Tanga
Mbunge
wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akisalimiana na wachezaji
wa timu ya Jang'ombe ya Zanzibar ambao wameweka kambi mkoani Tanga
wakati alipokwenda kukabidhi vifaa kwa timu ya African Sports.
SHARE
No comments:
Post a Comment