Baadhi
ya mashabiki wakifuatilia fainali ya Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu kati ya
timu za Qatajiring na timu Zahanati iliyochezwa katika kiwanja cha Dongobesh.(PICHA
NA ELEUTERI MANGI,WHUSM, MBULU)
|
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura
akiongea na Wananchi wakati wa kuhitimisha fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani
Mbulu.
Mbunge
wa Mbulu Vijijini Flatei Massay akiongea na Wananchi wakati wa kuhitimisha
fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (kulia)
akimkabidhi nahodha wa timu ya Qatajiring zawadi mbalimbali mara baada ya
kuibuka kidedea baada ya kuifunga timu ya Zahanati wakati wa fainali za Flatei
Jimbo Cup wilayani Mbulu. Katikati ni mdhamini wa mashindano hayo Mbunge wa Mbulu
Vijijini Flatei Massay.
NA
ELEUTERI MANGI, WHUSM, MBULU
HALMASHAURI
zote nchini zimetakiwa kutenga maeneo ya michezo wakati wa kupanga mipango miji
kwa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao.
Wito
huo umetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Anastazia Wambura alipokuwa akifunga fainali ya mashindano ya Jimbo Cup
inayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Mbunge wa Mbulu
Vijijini, Flatei Massay iliyochezwa katika eneo la kata ya Dongobesh Wilaya ya
Mbulu Mkoani wa Manyara.
“Natoa
wito kwa Halmashauri zote ikiwemo halmashauri yenu ya wilaya ya Mbulu wakati wa
kupanga matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya mipango miji mkumbuke kutenga
maeneo ya michezo, Baraza la Michezo la Taifa litatoa mafunzo ya michezo na
utaalam” alisema Naibu Waziri Wambura.
Akikabidhi
zawadi za washindi katika mashindano hayo ambao ni timu ya Qatajiring kutoka
kijiji cha tumati ambao ni mshindi wa kwanza na timu ya Zahanati kutoka kijiji
cha Diomati mshindi wa pili, Naibu Waziri Wambura amewahimiza wachezaji na
wananchi kuthamini michezo kwa kuwa ni ajira, inaleta umoja na mshikamano
miongoni mwa jamii.
Dakika
90 za fainali hizo ziliisha kwa timu zote kufungana bao 2-2 na hatimaye timu ya
Qatajiring iliibuka kidedea kwa ifunga timu ya Zahanati kwa penati 4-1.
Akionesha
umuhimu na umahiri wa wilaya ya Mbulu katika michezo, Naibu Waziri Wambura
amesema wilaya hiyo imekuwa kitovu cha wanamichezo bora hasa mchezo wa riadha
ambao wameiletea sifa Tanzania ndani na nje ya nchi.
Wanamichezo
hao ni pamoja na John Stephen Akhwari nguli mchezo wa riadha aliyeweka historia
ya kimataifa aliyewahi kusema “Nchi yangu haikunituma kuanza mashindano,
ilinituma kumaliza mashindano”Filbert Bai na wanaridha wengine.
Aidha,
Naibu Waziri Wambura amewashauri waandaaji wa mashindano hayo washirikishe pia
mchezo wa netiboli ili kuwaendeleza watoto wa kike katika mchezo huo.
Kwa
upande wake mdhamini wa mashindano hayo Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay
amesema kuwa alivutiwa kuanzisha mashindano hayo ili vijana wajihusishe na
michezo na kuboresha na kuendeleza afya zao na kuachana na masuala yanayoweza
kupoteza maisha yao na nguvu kazi ya taifa
Mashindano
hayo yalishirikisha timu 24 kutoka Mbulu Vijijini tangu kuanzishwa kwa mwezi
Julai mwaka huu na kufikia kilele Septemba 25 ambapo fainali ilichezwa katika
viwanja vya Dongobesh na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali na mashabiki lukuki
kutoka maeneo yote ya halmashauri hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment