MFUKO
wa Pensheni wa LAPF umekuwa mstari wa mbele kutoa misaada
mbalimbali kwa jamii ili kuharakisha maendeleo ya nchi na watu wake.
Mfano
wa hivi karibuni ni namna mfuko ulivyoitikia mwito kuchangia fedha kwa ajili
ujenzi wa ofisi za kisasa za walimu katika mkoa wa Dar es Salaam.
Itakumbukwa
kuwa ukosefu wa ofisi za walimu nchini ni tatizo kubwa ndiyo maana Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda amebuni mbinu ya kujikwamua na bila kuchukua
muda mrefu LAPF wakajitokeza haraka kusaidia.
LAPF
walitoa fedha taslimu Sh. Milioni 5 kwa mkuu huyo wa mkoa ili kuhakikisha suala
la ujenzi wa ofisi za kisasa kwa walimu mkoani humo linafanyika kwa haraka ili
waweze kuandaa ratiba/vipindi vya wanafunzi vizuri.
Mchango
ulitolewa kwa Mkuu wa Mkoa na Meneja Mawasiliano na Masoko wa LAPF, James Mlowe kwa ajili ya kununulia mifuko
500 ya saruji katika kuchangia kampeni ya ujenzi wa ofisi hizo za walimu kwa shule
za msingi na sekondari.
Meneja Mawasiliano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni
wa LAPF, James Mlowe akizungumza wakati wa tukio la kukabidhi msaada wa fedha
kwa ajili ujenzi wa ofisi za kisasa kwa walimu wa shule za msingi na sekondari
kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Ifahamike
kuwa kampeni hiyo ilianzishwa na Makonda katika jijini la Dar es Salaam,
ambapo ofisi zaidi ya 400 zitajengwa katika shule za jiji la Dar es
salaam hivyo kuboresha utendaji kazi wa walimu hao.
Kimsingi
LAPF imeonesha njia na wadau wengine wanatakiwa kuiga kwa kutoa misaada ya aina
hiyo ili kukuza maendeleo ya nchi hususan kwenye sekta ya elimu kwani ndiyo mkombozi
kwa watoto wetu.
Hii ina maana kuwa viongozi wa LAPF wameonesha kuwa wanathamini
sekta ya elimu kwa kiwango kikubwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment