Kampuni ya simu za mikononi ikiwa
chini ya kampuni mama ya TRANSSION HOLDINGS iliyopo China, imeachilia
rasmi simu janja “smartphone” mpya yenye kioo kamili/enea au kwa lugha
ya kiingereza (Full DISPLAY) yenye ukubwa wa uwiano “ratio” 18:9. TECNO
CAMON CM ni simu mpya kabisa kwa mwaka 2018 .
Mambo mengi yanatarajiwa na wadau kutoka katika simu hii mpya “CAMON CM” kwani ni muendelezo wa toleo lililopita la CAMON.
CAMON CM inabeba sifa kuu kubwa
ambayo ni kua na kioo enea/kamili “FULL DISPLAY” chenye uwiano wa 18:9,
kuifanya simu hii kua ya kwanza kutoka TECNO ambayo kioo chake hakina
mipaka au mikato kulinganisha na simu zingine zenye ukubwa wa 16:9.
Pia simu ina urefu wa nchi 5’7
ambayo itamuwezesha mtumiaji kutazama video, kucheza michezo “Games”,
kuperuzi mitandao kwa raha zaidi kulinganisha na simu ambazo zina
mipaka.
Camon CM inamonekano wa kifahari na umbo jembamba lenye ukubwa wa 7.75 mm.
Vigezo vingine ambavyo
vinapatikana kwenye CAMON CM ni pamoja na kamera bomba yenye uwezo wa
13MP kamera ya mbele na nyuma,4G LTE, RAM 2GB, ROM 16GB, na betri yenye
ukubwa wa 3000 mAh (Isiyotoka).
Simu hii ina rangi tatu ambazo ni “CITY BLUE”, MIDNIGHT BLACK na “CHAMPAGNE GOLD
CAMON CM sasa inapatikana,kwa taarifa zaidi tembelea http//www.tecno-mobile.com/tz
SHARE
No comments:
Post a Comment