NA
K-VIS BLOG, SAME
MKUU
wa wilaya ya Same, Bi. Rosemary Sitaki, amefurahishwa na kupanda kwa ufaulu wa
mtihani wa kidato cha nne 2017 ambapo ufaulu huo unaonyesha Wilaya imeshika
nafasi ya 21 kutoka nafasi ya 68 kitaifa na kimkoa imeshika nafasi ya nne
kutoka nafasi ya 6.
“Pongezi
kwa wote walioitikia wito wa kufanya mapinduzi haya, tukianza Na wanafunzi
wenyewe, walimu, idara ya elimu, ukaguzi,
Halmashauri kwa ujumla wao, CWT, taasisi za dini, NGOs, wazazi Na wote
tulioshiriki kwa namna yoyote ile.” Amesema Bi Sitaki wakati alipofanya ziara
ya kutembelea baadhi ya shule wilayani kwake.
Amesema,
ushirikiano huo umepelekea Wilaya ya Same kuona mapinduzi mazuri yaliyoanzia
shule za msingi na sasa Sekondari.
Lakini
pia amempongeza Mkuu wa Mmkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mngwira na timu yote ya
Mkoa kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwenye matokeo hayo.
“Kipekee
kabisa nitoe pongezi kwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli,. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutoa
elimu bila malipo, fedha za elimu na motisha inamchango mkubwa Hapo.” alisema
"Nawapongeza
wote mlioshiriki na wananchi wote wa Same; Na niwaombe matokeo haya yasitulaze
usingizi kwani dhamira yetu sio kuwa watu wa wastani ( average) Ila ni kufanya
vizuri kwa maendeleo ya wananchi wa Same Na Same ya baadaye"
Mhe.
Sitaki alimaliza kwa kusema " Same
is not same"
SHARE
No comments:
Post a Comment