WADAU
wa mradi wa kuwawezesha mabinti na wanawake vijana katika sekta ya
elimu wamekutana katikati ya wiki kujadili mpango kazi wa utekelezaji wa
mradi wa UNESCO kwa kushirikiana na UNWomen pamoja na UNFPA
unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Korea (KOICA).
Mradi
huo ambao umelenga kuondoa vikwazo vya elimu kwa wasichana na wanawake
kwa kuangalia sera, sheria na kanuni zinazowezesha maendeleo kwa
wanawake kwa kuzingatia matakwa ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya
kimataifa ambayo Tanzania imetia saini ulianza mwaka 2016.
Mradi
huo unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kwa
kusimamiwa na Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Wanawake la Umoja wa
Mataifa (UN Women) na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya Watu (
UNFPA) unatarajia kuiwezesha Tanzania kuwezesha elimu kwa kutumia mbinu
mtambuka kwa kutambua watu wa pembezoni. Kaimu
Mkuu wa ofisi na Mkuu wa kitengo cha Elimu ofisi ya Unesco Dar es
Salaam, Faith Shayo akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano wa
kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake
vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa wa Kitaifa
anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar es Salaam,
Mathias Herman.
Mradi
huo unatarajiwa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kuwa na uwezo
wa kuingia katika utuuzima bila kuvurugwa utaratibu wa upatikanaji wa
elimu.
Mradi huo unatekelezwa katika wilaya nne za Ngorongoro, Sengerema, Kasulu na Mkoani huko Pemba. Mkutano
huo wa kamati ya ufundi ya mradi ulilenga kutoa ratiba ya utekelezaji
wa mradi baada ya mada mbalimbali kuwasilishwa za utafiti uliofanyika na
hali halisi iliyopo nchini kuhusu wasichana na wanawake kwa kuangalia
sharia zilizopo, utamaduni na tabia.
Akizungumza
katika mkutano huo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Kitivo
cha Elimu, Dk. Felix Mulengeki alisema kwamba mradi huo utafanikiwa
kutokana na ukweli kuwa sharia na katiba za nchi zipo vizuri huku sera
nazo zikitambua haki ya kusoma. Ofisa
wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar
es Salaam, Mathias Herman akiwasilisha taarifa ya mwaka 2017 ya mradi
huo wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha
wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
Wakati
mradi unabuniwa ilionekana kwamba kutoeleweka kwa katiba na sheria
zilizopo zinazomlinda mtoto wa kike, uelewa hafifu umekuwa ukikwamisha
maendeleo kielimu kwa watoto wa kike. Dk.
Mulengeki alisema kwamba hali ya sera na sheria nchini Tanzania ni
salama zaidi kilichobaki utekelezaji wa mradi huo umelenga kukusanya pia
takwimu kwa ajili ya kutumika kutengeneza sera.
Katika mradi huo unatarajiwa kuongeza uelewa zaidi wa elimu ya afya ya uzazi na kutengeneza mifumo ya kuelimisha watu. Mada
mbalimbali zilizojadiliwa ziliwezeshwa kupata muda wa utekelezaji wa
vipengele mbalimbali ambavyo vilipaswa kufanyika ili kuondokana na tabia
mbaya ambazo zinamnyima binti wa Kitanzania kukamilisha elimu yake.Washiriki
wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake
vijana kujiendeleza kielimu wakifuatilia ripoti ya mwaka 2017 ya mradi
huo iliyokuwa ikiwasilisha Mathias Herman kwenye mkutano uliofanyika
katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.
Naye
Kaimu Mkuu wa ofisi na Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) ofisi za Dar es Salaam,
Faith Shayo amesema kwamba mkutano huo ni sehemu ya utekelezaji wa
mradi huo na kwamba kamati ya ufundi ya mradi huo ilikutana mara ya
kwanza Mei mwaka jana.
Naye
Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za
Unesco Dar es Salaam, Mathias Herman anasema kwamba kuna matokeo chanya
ya mradi huo. Anasema kwamba madhila
mengi ya mabinti katika wilaya hizo zinazofanyiwa utekelezaji wa mradi
yamepungua na hali zao kuwa bora kutokana na taasisi mbalimbali
zinazohusika na elimu na usalama wa watoto wakike kushirikiana kukabili
matatizo waliyonayo. Mhadhiri
Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Kitivo cha Elimu, Dk. Felix
Mulengeki akiwasilisha mada kuhusu sheria na taratibu zinazogusa elimu
ya watoto wa kike wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa
KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es
Salaam.
Pia
amesema katika suala la elimu ya afya ya uzazi na Ukimwi kumekuwa na
mabadiliko kwani taarifa zinakwenda kwa wakati na zinafanyiwa kazi
inavyotakiwa na sekta mbalimbali zikiwemo taasisi za kiserikali katika
kumsaidia mtoto wa kike Aidha amesema kwamba vitini vya kufundishia elimu mbalimbali ambazo zimo katika mradi zimeshafanyiwa kazi na kusambazwa. Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Socologia na
Anthropologia, Dk. Nandera Mhando akiwasilisha uchambuzi wa mradi wakati
wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana
na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam Mkuu
wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO Ofisi za Tanzania,
Christophe Legay (wa kwanza kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano
wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake
vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_3628" align="aligncenter" width="1404"] Mwakilishi
kutoka UN Women, Bi. Usu Mallya akifafanua jambo katika majadiliano
wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha
wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Mratibu
wa Elimu Shule za Msingi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Salvatory
Alute (katikati) akishiriki majadiliano wakati wa mkutano wa kamati ya
ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana
kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Unesco jijini Dar es Salaam. Afisa
Maendeleo wa Wilaya ya Ngorongoro, Teresia Irafay akitoa maoni wakati
wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana
na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Adam
Chacha kutoka kitengo cha Elimu ofisi za Unesco Dar es Salaam akiuliza
swali wakati wa mawasilisho ya mada mbalimbali katika mkutano wa kamati
ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana
kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Unesco jijini Dar es Salaam. Picha
juu na chini ni washiriki wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa
KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es
Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment