Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk.Mary Nagu, akihutubia wakati akifungua akifungua Kongamano la Wanawake na Uongozi 2018 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TGNP Mtandao, Vicensia Shule akizungumza kwenye kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akihutubia.
Profesa Bernadeta Killian akitoa mada kuhusu hali halisi ya wanawake na uongozi hapa nchini.
Spika wa Bunge Mstaafu Mama Anna Makinda na Naibu Waziri wa Walemavu (Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) – Stella Ikupa wakiwa kwenye kongamano hilo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye kongamano hilo.
Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk.Mary Nagu (katikati), akiwa na wadau wengine kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Taswira ya ukumbi kwenye kongamano hilo.
Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya akizungumza na wanahabari
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imeombwa kuendelea kutenga bajeti kubwa katika bajeti zake kwa ajili ya kumuendeleza mwanamke wa Tanzania.
Ombi
hilo limetolewa na Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk.Mary Nagu wakati
akifungua Kongamano la Wanawake na Uongozi 2018 jijini Dar es Salaam
jana.
"Tunaomba
bajeti ya serikali ibadilike kwa kuangalia ajenda ya jinsia ukizingatia
changamoto mbalimbali walizonazo wanawake" alisema Dk.Nagu ambaye
alikuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo.Dk.
Nagu aliwataka wanawake wote kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuzijua
changamoto walizonazo na kuzitatua kwa msaada wa viongozi wanawake
wastaafu.
Aliongeza kuwa wanawake ni jeshi kubwa na ndio wazalishaji wakubwa wa mali lakini
kwa namna moja hama nyingine wamekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ya
mali zinazotokana na uzalishaji wao kutumiwa na wanaume wao.
Katika
hatua nyingine Dk.Nagu aliomba wake wa maraisi wawe mbele kuwaendeleza
wanawake wenzao kama ilivyokuwa kwa Mama Anna Mkapa kupitia taasisi yake
ya Wote Sawa na Mama Salma Kikwete kupitia WAMA.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema wameamua kuandaa
kongamano hilo kama sehemu ya kutoa fursa kwa wanawake na wadau wengine
kutafakari wapi wamefanikiwa, wapi bado kama kunachangamoto na kupanga
mikakati ya kuimarisha ushiriki wa wanawake katika ngazi zote za maamuzi
pamoja na uongozi.
Alisema kongamano hilo pia litatoa fursa ya kutafakari suala la ushauri, ulezi au ukungwi katika kuimarisha uongozi.Alisema
tafiti zinaonesha kuwa nchi za Afrika zinapoteza takribani dola za
kimarekani 105 milioni kwa mwaka kwa kutowaingiza wanawake katika
uchumi, pia takwimu zinaonesha kuwa wanawake ni zaidi ya asilimia 70 ya
wakulima wadogo ambao ndio wanalisha nchi yetu.
Alisema
wanawake walioko katika sekta isiyo rasmi ni asilimia 51.1. ambapo
wanaume ni 48.9 na kuwa ni asilimia 20 tu ya wanawake ndio wanamiliki
ardhi.Katika
kongamano hilo walihudhuria viongozi mbalimbali wa serikali na wadau
wengine ambapo kauli mbiu ilikuwa ni "kusherehekea na kutambua Mchango
wa Uongozi wa Wanawake Jukwaani na Nyuma ya Pazia".
Mbunge
wa Bunda, Esther Bulaya amewata wanawake kuwa na moyo wa kuthubutu
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani wanauwezo wa kuongoza.
SHARE
No comments:
Post a Comment