Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
(MB) akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Afya na waandishi wa habari
wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya
mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
Mganga
Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi
Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) wakati akifungua mkutano wa wadau
wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
Meneja
mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya Dkt. Dafrossa Lyimo
akiwasilisha taarifa mbele ya Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati
wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
Mwakilishi
wa WHO Dkt. Ritha Njau akiwasilisha salamu za WHO wakati wa mkutano wa
wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
(MB) akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi
Wadau
wa Afya na Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka kwa Mgeni
rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya
kukinga saratani ya mlango wa kizazi
Picha
ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) wakati akifungua mkutano wa wadau
wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imedhamiria kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi nchini kwa kuwapa
kinga wasichana kuanzia umri wa miaka 9 mpaka 14 huku lengo likiwa ni
kuondoa tatizo hilo nchini.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akifungua mkutano wa
wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es
salaam.
“Katika
kukabiliana na ugonjwa wa Saratani na kuimarisha afya ya wanawake
Tanzania na kupunguza vifo vitokanavyo na Saratani , Wizara ya Afya
itaanza kutoa chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya Saratani ya mlango
wa kizazi”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri
Ummy aliendelea kusema kuwa kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya Ocean
Road Saratani ya Mlango wa kizazi zinazoongoza nchini kwa Asilimia 36
huku ikifuatia na saratani ya matiti, huku jumla ya wagonjwa wa Saratani
nchini katika kila wagonjwa 100, wagonjwa 46 ni wa Saratani ya mlango
wa kizazi na Saratani ya Matiti.
Aidhe,
Serikali imepanga kuanza na wasichana wenye umri wa miaka 14 kama umri
wa chini, huku ikitegemea kuchanja zaidi ya wasichana 610,000 katika
jitihada za kutokomeza kabisa tatizo hili la Saratani ya mlango wa
kizazi nchini,
Mhe
Ummy alisisitiza kuwa Chanjo hii itatolewa katika vituo vyote vya Afya
nchini vya Serikali, vya watu binafsi na vikundi mkoba bure, na
kuwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha mabinti zao wanapata chanjo hii
ili kujikinga na ugonjwa huo.
Nae
Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dafrossa Lyimo aliendelea kuwatoa hofu
wananchi na kusisitiza juu ya umuhimu wa kinga kuliko tiba na kusema
kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na shirika la Afya duniani
na mamlaka ya chakula na viodozi nchini (TFDA).
SHARE
No comments:
Post a Comment