Makubaliano
hayo yalifikiwa jana, wakati Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipokutana
na uongozi wa juu wa kampuni hiyo wizarani mjini Dodoma.
Aidha,
makubaliano mengine yaliyofikiwa katika kikao hicho ni kuwa, kazi za awali za
maandalizi ya ujenzi ziwe zimekamilika ifikapo mwezi Machi mwaka huu.
"Ni
lazima tuharakishe mchakato huu kama Mheshimiwa Rais Magufuli alivyoagiza.
Hivyo, tumekubaliana kwamba shughuli zote za maandalizi ziwe zimekamilika
ifikapo Machi mwaka huu ili kuwezesha shughuli rasmi za ujenzi wa Bomba kuanza
mwezi Mei," alifafanua Waziri Kalemani.
Vilevile,
katika kikao hicho, Rais wa Kampuni ya Total, Sehemu ya Afrika, Guy Maurice
ambaye alikuwa kiongozi wa Ujumbe huo, alibainisha nia ya kampuni yake kuwekeza
katika shughuli nyingine mbalimbali zinazohusiana na Mradi wa Bomba, jambo
ambalo alisema litainufaisha zaidi Tanzania.
Mbali
na makubaliano yote yaliyofikiwa, Waziri Kalemani pia alisisitiza kuwa ni
muhimu kampuni ya Total iwasilishe Mpango-Kazi wake wizarani mapema
iwezekanavyo ili utumike kama mwongozo-rejea katika kutathmini utekelezaji wa
Mradi huo mkubwa.
Kampuni
ya Total ndiyo mwekezaji katika utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Bomba la
Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga.
Kikao
hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi
Mwinyimvua, Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli Mhandisi Innocent Luoga,
Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi Lusius Mwenda, Mkurugenzi wa Sera na Mipango
Haji Janabi na maafisa wengine waandamizi kutoka wizarani.
SHARE
No comments:
Post a Comment