Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (kushoto) akizungumza katika kikao cha
kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse
(kulia) ameongoza ujumbe huo uliokuja kwa ziara ya mafunzo nchini
Tanzania.
Baadhi ya maofisa waandamizi
kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini wakiwa kwenye
kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi ya Lesotho na
Tanzania.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale akielezea namna
TANROADS inavyotekeleza kazi zake kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu
na wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. Ujumbe huo unaongozwa na
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse
pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho,
Mathabathe Hlalele.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Eng. Joseph Nyamhanga
(kulia) akisalimiana na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mathabathe Hlalele
(kushoto) mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano za jijini Dar es Salaam katika ziara ya mafunzo.
Katikati ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo
Moramotse.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi wa nchi ya Lesotho, Mathabathe Hlalele (katikati) akizungumza
kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi hiyo na
Tanzania.
Baadhi ya maofisa waandamizi
kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi nchini Lesotho wakiwa katika kikao
cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi hiyo na Tanzania.
Baadhi ya maofisa watendaji wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) wakieleza namna ya utekelezaji
miradi mbalimbali iliyo chini ya wakala hiyo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa
Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse (kulia) akizungumza katika kikao cha
kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania.
Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias
Kwandikwa akiwa katika mazungumzo hayo.
Kikao cha wajumbe hao katika ofisi za Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kikiendelea.
SHARE
No comments:
Post a Comment