Mkuu wa Idara ya Mifugo Uvuvi
katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Dk. Alphonce Bagambabyaki
akishiriki katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe.
Wananchi wakishiriki katika zoezi la upigaji chapa ng’ombe katiia kijiji cha Wishiteleja kata ya Mondo.
Moja wa ng’ombe akiwa tayari amepigwa chapa katika sehemu ya mguu.
………………………………………………………………………..
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Kishapu
imeweza kupiga chapa jumla ya ng’ombe 225,131 katika zoezi la utambuzi
na usajili wa mifugo linalofanyika katika kata zote zenye wafugaji
wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo, Stephen Magoiga amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na
limeweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa pamoja na kuwepo kwa changamoto
kadhaa.
Alisema zoezi hilo ni agizo
kutoka serikalini na kinachofanyika ni kulitekeleza kwa kiwango
kinachotakiwa na kuweza kuwafikia wafugaji katika maeneo mbalimbali
katika kata za wilaya hiyo.
“Zoezi la upigaji chapa ng’ombe
tulilipokea na tumeweza kulitekeleza ingawa zipo changamoto mbalimbali
zikiwemo baadhi ya maeneo kutokuwepo kwa wafugaji tumefanikiwa kuifikia
mifugo hiyo,” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya
Mifugo Uvuvi katika Halmashauri hiyo, Dk. Alphonce Bagambabyaki alisema
Wilaya imeweza kufikia lengo hilo kwa zaidi ya asilimia 75 ya lengo
ambalo ni ng’ombe laki tatu.
Alisema vijiji lengwa vyote 125
vimeweza kufikiwa na ingawa zipo baadhi ya changamoto kama imani potofu
kwa baadhi wafugaji kuwa huenda wakachukuliwa mifugo yao pindi
wanapoifikisha vituo vya zoezi la upigaji chapa.
Zoezi hilo lilianza rasmi Oktoba
20 mwaka jana ambapo lilizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mh.
Nyabaganga Taraba linataka mifugo yote nchini kutambuliwa kwa kutumia
chapa chini ya sheria ya utambuzi namba 12 ya mwaka 2010.
Aidha, zoezi hilo limekuwa
likitekelezwa na wataalamu wa mifugo kutoka wilayani makao makuu
wakishirikiana na wataalamu wa kata na vijiji mbalimbali ili kuhakikisha
limekwenda kwa ufanisi.
Wakati akizindua zoezi hilo Mh.
Taraba alibainisha kuwa zoezi la utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa
ng’ombe kwa kutumia chapa litapunguza changamoto zinazowakabili
wafugaji.
Alibainisha kuwa Kishapu ni
miongoni mwa wilaya ambazo baadhi ya wafugaji wake wanakabiliwa na
matatizo yakiwemo wizi wa mifugo katika unaoweza kutokea katika maeneo
mbalimbali nchini.
Pia linasaidia kupunguza migogoro
migogoro baina ya wakulima na wafugaji wanaokuwa wanahama hama bila
kufuata utaratibu maalumu kwa lengo la kutafuta malisho kwa ajili ya
mifugo yao.
SHARE
No comments:
Post a Comment