KAIMU mkurugenzi halmashauri ya
Mkuranga, Mkoani Pwani,ambae pia ni afisa maendeleo ya jamii,Safina
Msemo akimshukuru mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani, Zainab Vullu
(kushoto aliyesimama)kwa kuchangia baadhi ya mifuko ya saruji kati ya
mifuko 70 na malumalu vipande 500 vilivyogharimu zaidi ya mil.1.6
MBUNGE wa viti maalum
Mkoani Pwani, Zainab Vullu, akimkabidhi kaimu mkurugenzi halmashauri ya
Mkuranga, Mkoani Pwani,ambae pia ni afisa maendeleo ya jamii,Safina
Msemo (mwenye gauni la kitenge) baadhi ya mifuko ya saruji kati ya
mifuko 70 na malumalu vipande 500 alivyochangia ambapo vimegharimu zaidi
ya mil.1.6.
Picha na Mwamvua Mwinyi
………………
Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
MBUNGE wa viti maalum
Mkoani Pwani,Zainab Vullu amekabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji
pamoja na malumalu vipande 500 ,vilivyogharimu sh .milioni 1.6 ,katika
halmashauri ya Mkuranga.
Kati ya vifaa hivyo
mifuko 50 ya saruji ni mchango katika ujenzi wa nyumba ya mganga
zahanati ya Kijiji cha Koma na mifuko mingine 20 ujenzi wa nyumba ya
mwalimu shule ya msingi Kisiju Pwani.
Vullu alielekeza
,Malumalu (tiles)zipelekwe shule ya msingi Kisiju Pwani,katika ujenzi wa
vyoo lakini aliomba kipaombele kipewe kwenye vyoo vya wanafunzi wa kike
ili kujihifadhi wakati wakiwa katika hedhi .
Aidha alisema
anahamasisha ujenzi wa nyumba ya mganga na aliwataka wadau wengine
waunge mkono jitihada za serikali ,halmashauri ,mbunge wa Mkuranga
Abdallah Ulega aliyechangia mifuko 100 ya saruji .
Hata hivyo,Vullu
alisema kilichomgusa kuchangia pia ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi
inaelekeza kusimamia maisha na maslahi ya mtanzania .
“Kijiji cha Koma
hakina zahanati ,kutokana na suala hilo niliona nguvu za Mbunge
,halmashauri na ndipo Jan 1 ,nikwenda kuona hali ilivyo ,nimeona nitoe
fedha za mfukoni mwangu nichangie mifuko ya saruji ujenzi wa nyumba ya
mganga .”
“Vijiji vya huko ni
kisiwa ,ukitaka kufika lazima ukitoka ngambo hii hadi nyingine utumie
lisaa hadi limoja na zaidi ,wakazi hao wakihitaji huduma zaidi za kiafya
inabidi wakimbilie hospital ya wilaya ya Mkuranga ambako ni umbali
mrefu “alisema Vullu .
Vullu alisema suala
la afya ni muhimu hivyo kuna kila sababu ya kukamilisha ujenzi huo wa
zahanati na nyumba ya mganga ili wananchi waondokane na kero yakufuata
huduma za afya mbali .
Nae kaimu mkurugenzi halmashauri ya Mkuranga, ambae pia ni afisa maendeleo ya jamii ,Safina Msemo alishukuru kupata mchango huo.
Safina alisema kwa niaba ya halmashauri, alisema vifaa hivyo vitasaidia kuongeza nguvu kwenye ujenzi huo .
Kwa upande wake
,mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kisiju Pwani, mwl.Jofrey Mbwale ,alitoa
shukrani zake na kusema shule hiyo bado inakabiliwa na uhaba wa nyumba
za walimu sita .
Alisema kuna walimu nane nyumba zilizopo ni mbili huku alieleza kuna mahitaji ya walimu 20 .
Mwl.Mbwale alieleza mahitaji katika matundu ya vyoo ni matundu 41 yaliyopo ni 20 .###
SHARE
No comments:
Post a Comment