Chanzo, VOA Swahili.
Tarehe 4 mwezi Ferbuari ni siku ya saratani duniani ambapo kila mwaka inatoa fursa ya kuongeza uwelevu wa saratani na kushawishi njia za kuizuia, kuitambua na matibabu. Katika eneo la utambuzi, watafiti katika chuo kikuu cha Johns Hopkins kwenye kitengo cha Kimmel Cancer kilichopo Baltimore, Maryland wamefanya utafiti wa upimaji damu ambao unasaidia kutambua aina nane tofauti za saratani. Saratani ni ugonjwa wa pili wa juu unaosababisha kifo duniani kote, na watu wengi hawatambui kuwa wana maradhi hayo mpaka pale dalili zinapojitokeza. Hili linaweza kubadilika kwa kupima damu ambayo hujulikana kama CancerSEEK.
SHARE
No comments:
Post a Comment