Mwakilishi
wa kampuni ya TatuMzuka,Milard Ayo akizungumza mbele ya Waandishi wa
habari mapema jana jijini Dar,alipokuwa akiwatambulisha washindi wa
TatuMzuka Daily,waliojinyakulia Milioni 10 wakiwemo wapenzi walioingia
kwenye kampeni ya Valentine iliobeba kauli mbiu ya ‘Ukishinda,
Unayempenda naye Anashinda’.Pichani kulia ni washindi wa kampeni ya
Valentine Jumanne Kabwe na Mariam Omary ambao wote kwa pamoja
walijishindia milioni 10 na kushoto ni Nicolaus Chilipweli
aliyejishindia milioni 10.
Pichani
kushoto ni Mshindi wa TatuMzuka Daily,Nicolaus Chilipweli mkazi wa
Bagamoyo akielezea namna alivyojishindia Kitita cha Milioni 10 kupitia
mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka na namna atakavyozitumia fedha hizo.
Pichani ni washindi wa kampeni ya Valentine waliotimiza kauli mbiu ‘Ukishinda, Unayempenda naye Anashinda’ Jumanne Kabwe na Mariam Omary ambao wote kwa pamoja walijishindia milioni 10
Kampuni
ya mchezo wa bahati nasibu, Tatu Mzuka ilizindua kampeni mpya ya
Valentine, ambayo ilianza rasmi hivi karibuni mpaka Februari
18,2018.Kampeni hiyo yenye kauli mbiu, ‘Ukishinda, Unayempenda Naye
Anashinda’ imelenga kuhakiksha inashamirisha msimu wa Valentine kwa
watanzania kupata fursa ya kujishindia mamilioni lakini pia wawapendao
pia kupata fursa ya kushinda.
SHARE
No comments:
Post a Comment