Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa (kulia)
wakimsikiliza Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba
Cashew, Abdulrahman Sinani, wakati alipotembelea kiwanda hicho,
kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara, Gelasius Gasper Byakanwa, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa (katikati)
wakiangalia mashine ya kubangulia korosho katika Kiwanda cha Korosho cha
Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara,
kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani,
Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mbanguaji korosho Zuhura Abdallah,
katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani
Tandahimba, Mkoani Mtwara, katikati ni Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa
na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper, Februari 28,
2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa mashine ya kuchambua korosho na Meneja
Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani katika Kiwanda cha
Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani
Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa mashine ya kukaushia korosho na
Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani katika Kiwanda
cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani
Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia ubora wa korosho, iliyo teyari kuliwa,
wakati alipotembelea Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew,
kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri
Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa Mtwara kupambana na
makundi ya watu yanayotaka kuharibu masoko ya korosho.
Hatua
hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mnunuzi aliyekataa kununua korosho
kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha ubora wa korosho alichokikuta
ghalani.Ametoa
agizo hilo leo (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati akizungumza na
watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.
“Tandahimba
korosho zote ni daraja la kwanza sasa korosho chafu zinatoka wapi? Kuna
kundi linataka kuharibu soko lazima tupambane nalo.”Waziri
Mkuu ameongeza kuwa “lazima mshirikiane kuwabaini walioleta korosho
chafu Tandahimba na wakipatikana wachukuliwe hatua kali za kisheria.”
Amesema
haiwezekani mnunuzi amenunua korosho daraja la kwanza alafu anakuja
anakuta korosho nyingine tena chafu, lazima waliozibadilisha wasakwe. Awali,
Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Amama Farms,
ambapo ametoa wito kwa walionunua viwanda vya korosho wafunge mashine
mpya na kuanza uzalishaji.
Hata
hivyo amewataka wamiliki wa viwanda vyote vya kubangulia korosho
washirikiane na Serikali katika kufuata utaratibu wa kununua korosho.Pia
Waziri Mkuu amezindua barabara yenye urefu kilomita tatu iliyojengwa
kwa kiwango cha lami ambayo imegharimu sh. bilioni 1.38 zilizotokana na
mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.
Kwa
upande wake Meneja wa Kiwanda hicho Kwa Mahmoud Sinani alisema korosho
zinazobanguliwa kiwandani hapo zinauzwa ndani na nje ya nchi.Amesema
katika awamu ya kwanza ya uwekezaji huo umegharimu sh. bilioni 12 na
wanatarajia kuendelea na awamu ya pili ambapo watawekeza dola milioni
20.
Amesema
kwa sasa kiwanda hicho kimeajiri watumishi 250 na wanatarajia kuajiri
watumishi 1,500 mara baada ya kumaliza awamu ya pili ya upanuzi wa
kiwanda.Pia
Waziri Mkuu amewapongeza watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya
Tandahimba kwa kuweka kipaumbele katika ujenzi wa miundombini ya
barabara kwa kiwango cha lami.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 28, 2018.
SHARE
No comments:
Post a Comment