Zaidi
ya madiwani 20, kutoka mikoa mitano na wilaya Nane wamekutana jijini
Dar Es Salaam, kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana
na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.
Madiwani
hao ni kutoka Halmashauri za wilaya za Kishapu (Shinyanga), Tarime
(Mara), Mbeya (Mbeya), Morogoro Vijijini (Morogoro) na manispaa za
Ilala, Kinondoni na Ubungo (Dar es salaam).
Madiwani
hao ambao walikutana katika ofisi za TGNP Mtandao, zilizopo Mabibo Dar
Es Salaam, pia walipata nafasi ya kutembelea Kipunguni na kujionea mradi
unaotekelezwa katika eneo hilo.
Pamoja
na kujifunza masuala mbalimbali, Madiwani hao walipata fursa ya
kushirikisha masuala ya kijinsia ambayo bajeti za Halmashauri zao
zimezingatia na jinsi walivyofanikiwa kutenga rasilimali za kuhakikisha
bajeti zao zinakidhi mahitaji ya kijinsia.
Wakiwa
kata ya Kipunguni iliyopo manispaa ya Ilala madiwani hao walikutana na
Diwani wa Kata hiyo na kujifunza jinsi ambavyo wananchi waliopo katika
Kituo cha Taarifa na Maarifa walivyofanikiwa kuleta maendeleo kwa
kushirikiana na viongozi ikiwepo kupambana na ukatili wa kijinsia hasa
ukeketaji.Eneo
hilo maarufu kwa wakazi wa kutoka mikoa ya kaskazini ambako yapo
makabila yanayofanya ukeketaji nalo limekumbwa na tatizo hilo.
Aidha
katika ziara hiyo, waheshimiwa madiwani walipata nafasi ya kujifunza,
faida za mabunge ya jamii, na kujifunza miradi ya maendeleo ya kuwezesha
wananchi kiuchumi ambayo inatekelezwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana
na wananchi wa Kipunguni.
Katika
mabadilishano ya uelewa mmoja wa wajumbe ambaye ni Diwani wa Ijombe
wilayani Mbeya, Stimar Hepa John alisema kwamba wakati umefika kwa
wananchi wengi kutambua shughuli za TGNP Mtandao.
Alisema
awali alikuwa akidhani kwamba asasi hiyo ina mlengo wa kisiasa kiasi
cha kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwao lakini baada ya elimu
hii amebadili uelekeo na kuitaka taasisi hiyo kupeleka elimu Tanzania
nzima.
Alisema,
"Anaona kwamba TGNP ina jukumu kubwa nchini Tanzania na hivyo
inastahili kuwa kila mahali kuwasaidia watanzania kujiimarisha katika
nyanja zote."Diwani
huyo wa Ijombe ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Igawii alisema
pamoja na kubadili mwelekeo aliwataka wabunge kuona kwamba wanapoandaa
miradi hawaandai mbunge mpya bali kusaidia wananchi kujiinua kiuchumi.
Katika mkutano huo walitoa maazimio kadhaa ya kufanyiwa kazi katika halmashauri.Miongoni
mwa maazimio hayo ni namna ya kusimamia Mfuko wa Maendeleo wa wanawake
kuhusu ile asilimia 5 na kutekeleza dhana ya viwanda.
Kwa
mujibu wa Ofisa Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba mambo
mengine waliyokubaliana ni kushawishi na kufuatilia ongezeko kila
zahanati na vifaa vya kujifungulia na kuhimiza uwekaji wa mikakati ya
kupambana na ukatili wa jinsia na kuunda kamati za ulinzi za mtoto.
Pia
imeelezwa haja ya TGNP Mtandao kuendelea kutoa elimu kwa kusaidiwa na
mabaraza ya halmashauri kuhusu rasilimali fedha na kufuatilia uwekezaji
katika ujenzi wa hosteli kupunguza umbali wa watoto wa kike kutembea
kufuata shule.Mambo
mengine ni kuona kwamba uandaazi wa bajeti unaanzia ngazi ya kijiji au
mtaa badala ya kata na kukosekana kwa sauti za wananchi katika bajeti.
TGNP
Mtandao ni asasi ya kiraia inayo fanya kazi na wanajamii kwa kipindi cha
miaka 25 sasa, kwa kipindi chote hicho kimeshirikiana na taasisi za
serikali, Wizara, Halmashauri na Kamati za Bunge za kisekta kwa ajili ya
majadiliano, mashauriano na mafunzo ya namna ya kuboresha huduma za
jamii kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Ofisa
Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba akifafanua jambo wakati
akiendesha mjadala kwa Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8
walioshiriki mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya
kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao
uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani
wa Kata ya Songwa wilayani Kishapu, Shinyanga, Ngoromole Abdul
akibadilishana uzoefu na madiwani wenzake wakati wa mkutano wa
kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi
katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na
kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani
wa Ijombe wilayani Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari
Igawii, Stimar Hepa John akichangia kwenye mjadala wakati wa mkutano wa
kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi
katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na
kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.Diwani
wa Kata ya Mshewe ya Wilaya ya Mbeya vijijini, mkoani Mbeya, Esther
Mbega akishiriki kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana
uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta
maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Diwani
wa Kata ya Ukenyenge ya wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Anderson
Mandia akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na
kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo
katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi
wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Pichani
juu na chini ni washiriki wakiendelea kujadiliana wakati wa kipindi cha
maswali na majibu katika mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza
jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata
zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Sehemu
ya Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8 walioshiriki mkutano wa
kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi
katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na
kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment