Mwenyekiti
wa Jumuiya wa Makanisa ya Pentekoste,(Katikati) ambaye pia ni Askofu
wa Huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu Godfrey
Malassy alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es
salaam.
Na Skolastika Tweneshe-MAELEZO
Fedha
zitakazopatikana katika Tamasha la mkesha wa kuombea amani nchini
zitatumika kuwasaidia watu wenye mahitaji hasa afya ya mama na mtoto.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya wa Makanisa ya Pentekoste , ambaye
pia ni Askofu wa huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu
Godfrey Malassy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam.
Malassy
alisema kwamba, fedha zitakazopatikana katika tamasha hilo zitanunua
vifaa vinavyotumia nishati ya jua (solar Panels) ili kuwasaidi wamama
wajawazito na watoto wanaozaliwa.
“Kina
mama wajawazito na watoto wanakufa mahospitalini kutokana na kukosa
umeme hasa vijijini, hivyo tumeamua fedha zitakazopatikana mkesha huu
tutanunua solar” alisema Malassy
Aidha
Askofu Malassy amewaomba wananchi kuzidi kumuombea Rais John
Magufuli katika kuliongoza Taifa la Tanzania ili aendelee kufanya kazi
yake kwa ufanisi ambayo tayari imekubalika ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti
huyo alitambulisha kitabu kiitwacho IJUE SIRI YA AMANI KWA TAIFA
ambacho kinauzwa Sh.5000 amesema kuwa kitabu hicho kina lengo la
kuelimisha thamani na jukumu la watanzania kuilinda Amani bila kujali
itikadi za dini, siasa wala ukabila
Pia
ameomba kwa atakaeguswa na matatizo yanayowakumba wamama wajawazito
anaweza kutuma mchango wake kwa namba
zifuatazo 0755202204, 0719202204, 06842022 04.
Mkesha
huo ni wa 18 tangu uanze kufanyika na mwaka huu utafanyika katika
Uwanja wa Uhuru usiku wa tarehe 31 ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa
Awamu ya Tano Mhe. John Pombe Magufuli.
Wachungaji
mbalimbali wa Makanisa ya Pentekoste wakiwa katika mkutano na Waandishi
wa Habari kwaajili ya kuzungumzia mkesha utakaofanyika Desemba 31.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa
ya Pentekoste, (Hayupo pichani) ambaye pia ni Askofu wa huduma ya
Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu Godfrey Malassy alipokuwa
akizungumza leo Jijini Dar es salaam. Picha zote na Ally Daud MAELEZO.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment