Wananchi wa Kata ya Nyengedi
Lindi wakimsikiliza Mh. Nawanda DC wa Lindi akiwaelimisha umuhimu wa CHF
katika kampeni ya uhamasishaji unaofanywa na NHIF kwa kushirikiana na
Halmashauri ya Wilaya hiyo
Mkuu wa wilaya ya Lindi Mh. Yahya
Nawanda akiwasikiliza akisikiliza kwa makini hoja za wana Nyengedi
ili kupata mrejesho wa huduma za afya katika kata hiyo.
wakati alipokuwa akiwaelimisha kuhusu umuhimu wa huduma za CHF katika
kampeni ya uhamasishaji inayofanywa na NHIF kwa kushirikiana na
Halmashauri ya Wilaya hiyo
Mkuu wa wilaya ya Lindi Mh. Yahya
Nawanda akisisiztiza jambo wakati NHIF ilipozindua kampeni hizo
katika wilaya ya Lindi mkoa wa Lindi kulia ni Mkuu wa mkoa huo Mh.
Jordan Lugimbana na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi
Mzee Ali Mtopa na Eugine Mikongoti Mkurugenzi wa wa Huduma na Uendeshaji
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF
Wana Nyengedi wakipima ili kujua afya zao katika kampeni ya CHF.
Wanakijiji wa Nyengedi
wakidunduliza fedha ili kufikisha mchango wa sh. 10,000 kwa kaya ili
wajisajili na CHF baada ya kuhamasika.
…………………………………………………………………………………..
Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya kwa kishirikiana na Halmashauri ya Lindi Vijijini wameendelea na
kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii
CHF katika kata ya Nyangedi.
Katika uhamasishaji huo
uliongizwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Nawanda kaya 70 zilijiunga papo
hapo kwa kuchangia Shilingi 10,000 kwa kaya hivyo jumla ya Shilingi
700,000 zilikusanywa.
Aidha Mh. Nawanda
alimwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha hakuna upungufu wa dawa
katika kituo hicho na endapo litatokea hilo wananchi wamjulishe mapema.
Pia aliwakumbusha maagizo ya Mkuu wa Mkoa kwamba wasiojiunga na CHF watalipia Sh. 10,000 kwa matibabu kila wanapoenda kutibiwa kama hawaoni umuhimu wa kuchangia 10,000 kwa kaya kwa mwaka mzima na wakatibiwa kwa kadi.
Alimaliza kwa kuwahimiza watu kufanya kazi kwa bidii ili waweze kutimiza mahitaji yao kama afya kwani fursa za uzalishaji zipo.
Uhamasishaji wa CHF unaendelea katika kata mbalimbali za Lindi katika wiki hìi na baada ya hapo katika Halmashauri mbalimbali nchini.

SHARE
No comments:
Post a Comment