Mwonekano wa Ofisi za Daraja la Kigamboni zitakazotumiwa na wasimamizi wa daraja hilo linalotarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi Machi mwaka huu.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano sehemu ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga amesema daraja la Kigamboni
litaanza kutumika kuanzia Machi mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kukagua hatua
za ujenzi wa daraja hilo Eng. Nyamhanga amemtaka msimamizi wa ujenzi huo kuhakikisha
hatua ya ujenzi iliyobaki inakamilika katikati ya mwezi februari na kuanza kazi
mwanzoni mwa mwezi Machi.
“Hakikisheni Machi mosi magari yaanze
kupita rasmi kwenye daraja hili na hivyo kufungua ukurasa mpya kwa wakazi wa Kigamboni
ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na msongamano katika eneo la Magogoni”,
amesema Eng. Nyamhanga.
Eng. Nyamhanga amesisitiza kuwa Serikali
inaangalia uwezekano wa kuunganisha daraja la Kigamboni na barabara ya Charambe,Mlandizi
hadi Chalinze ili kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji.
Amemtaka meneja wa mradi wa ujenzi wa
daraja hilo toka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eng. John Msemo kuhakikisha
anatafuta Wakala makini atakayesimamia na kuendesha mradi huo.
Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita
680, unasimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS) na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano linatarajiwa kuishi
zaidi ya miaka 100 na kuwa na uwezo wa kupitisha mizigo ya tani 56
zinazokubalika katika nchi za jumuiya ya madola.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
SHARE








No comments:
Post a Comment