Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (wapili kushoto) akiwasili Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
ziara ya kikazi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Balozi Hassan Simba, kulia ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha. Katika hotuba yake, Rwegasira
alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze
kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato.
Mkuu
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha
(kulia) akitoa taarifa ya utendaji wa Jeshi lake kwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(katikati) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao
Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Rwegasira
alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze
kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
wakiongozwa na Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (wapili kulia) wakati
Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo, Mtaa wa
Lumumba jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Rwegasira
alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze
kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Wapili kushoto ni Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba. Kulia ni Fikiri Salla,
Kamishna wa Usalama kwa Umma Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Rogatius Kipali (kushoto).
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba
(wapili kushoto) akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji wakiongozwa na Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kulia) wakati
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati)
alipoambatana na Naibu Katibu Mkuu huyo katika ziara ya kikazi Makao
Makuu ya Jeshi hilo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo. Katika
ziara hiyo, Katibu Mkuu, Meja Jenerali Rwegasira alilipongeza jeshi hilo
kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika
ukusanyaji wa mapato. Kushoto ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo,
Rogatius Kipali.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi
Hassan Simba (kulia) wakiwa na maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
wakiongozwa na Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (watatu kulia),
wakizungumza jambo mara baada ya Katibu Mkuu huyo kumaliza kulikagua
jengo la ghorofa tano la Ofisi za Makao Makuu ya jeshi hilo, lililopo
Tazara Mchicha jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Rwegasira alilipongeza
jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi
katika ukusanyaji wa mapato. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
SHARE
No comments:
Post a Comment