Rais 
wa Shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akiwa na Mwe3nye3kiti wa
 Chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro,( KAA) Liston Methacha wakati wa 
uzinduzi rasmi wa mbio za Dodoma Hapa Kazi tu Half Marathoni 2016 
zinzotarajia kufanyika January 30 mwaka huu mjini Dodoma. 
Baadhi
 ya wadau wa Riadha wakifuatiia mkutano wa uzinduzi wa Mbio za Dodoma 
Hapa kazi tu Half Marathon 2016 uliofanyika katika Hotel ya Nyumbani 
mjini Moshi. 
Rais 
wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza na 
wanahabari (hawako pichani ) wakati wa uzinduzi rasmi wa Mbio hizo. 
Kocha 
wa timu ya taifa ya Riadha ,Francis John akiwa na wanariadha ,Alphonce 
Felix na Said Makula waliofuzu viwango vya kushiriki mashindano ya 
Olyipiki ,walipotamburishwa mbele ya wanahabari . 
Raisi wa RT ,Mtaka kifanya mahojiano na Mwandishi wa habari ,Enos Masanja wa Azam TV.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SHIRIKISHO
 la Riadha Tanzania(RT) limeandaa mbio fupi kwa ajili ya kuhitimisha 
siku 100 za rais Dk.John Pombe Magufuli kuwa Ikulu zitakazotimua vumbi 
jumamosi hii januari 30 mwaka  huu mjini Dodoma.
Mbio 
hizo zimepewa jina maalumu la Dodoma ‘hapa kazi tu’ Half Marathon ambazo
 zitashirikisha washiriki mbali  mbali wakiwamo waheshimiwa 
wabunge,mawaziri,wanafunzi,walemavu na wanariadha wakongwe nchini.
Akizindua
 mbio hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki zinazodhaminiwa na Kampuni ya 
JSM,Rais wa shirikisho hilo,Anthony Mtaka alisema kuwa lengo la 
kuanzishwa kwa mbio hizo ambazo zimeandaliwa na kuendeshwa na shirikisho
 hilo ni kufufua michezo hapa nchini.
Pia 
alisema mbio hizo zitatumika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe 
Magufuli kutimiza siku 100 tangu aingie maradakani ambazo zitakuwa 
februari 14 mwaka huu.Kwa mujibu wa rais huyo wa RT,mbio hizo 
zimegawanywa katika makundi matatu ambako mbio za kwanza ni za kilomita 
2.5 ambazo zitashirikisha wabunge,mawaziri,walemavu,wanafunzi ,wazee na 
watu mbalimbali.
Mbio 
za kilomita 5 ambazo ni za kujifurahisha zitashirikisha wakimbiaji wote 
na mbio za nusu marathon ambazo zitakuwa ni mbio za ushindani washindi 
watapata zawadi .Akitangaza zawadi  kwa washindi,Mtaka alisema mshindi 
wa kwanza kwa upande wa wanaumme na 
wanawake
 atapata zawadi  ya piki piki yenye thamani ya sh,Milioni 2.8,mshindi wa
 pili akipata bati 100,wa tatu bati 40,mshindi wa nne akipata sh,200,000
 huku mshindi wa tano akiondoka nash,100,000.
Mshindi
 wa sita hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha sh,50,000 kila mmoja 
huku waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa  ndiye atayakuwa mgeni rasmi 
katika ufunguzi wa mbio hizo na atashiriki  mbio za kilomita 2.5.
Wanafunzi
 waatakaopenda kushiriki mbio hizo watasajiliwa kwa sh,500,huku vwasio 
wanafunzi wakisajiliwa kwa sh,1,000 na wingine ambao hawakutajwa ni 
kundi gani wakisajiliwa kwa sh,5,000 na fedha hizo kwa mujibu wa Mtaka 
zitasaidia kambi ya wanariadha watakaoshiriki michuano ya Olimpiki.
Uzinduzi
 huo pia ulitumika kuwatambulisha wanariadha wawili ambao wamekidhi 
vigezo vya kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil 
mapema mwezi Agosti mwaka huu  ambako nchi zaidi ya 216  kutoka kila 
kona ya dunia zitashiriki.
Wanariadha
 hao ni Alphonce Felix ambaye ana wastani wa muda wa kukimbia wa saa 
2:12.01 na Said Makula ambaye muda wake wa kukimbia ni saa 2:13.27 na 
watatumia mbio hizo mjini Dodoma kama majaribio yao ya kitaifa kati ya 
majaribio sita ya kitaifa kabla ya kwenda Brazil.
Julai 6
 mwaka jana,Felix alishiriki mbio za Gold Coast Marathon nchini 
Australia na kumaliza nafasi ya sita huku Makula akishiriki mbio za 
Casablanca Marathon oktoba 25 mwaka jana  na kumaliza katika nafasi ya 
nne. 
  SHARE 
  














No comments:
Post a Comment