Vero Ignatus - Moshi Kilimanjaro.
Chama cha
Karate Mkoa wa Kilimanjaro wanaiomba serikali kutupia macho kwenye
mchezo huo kwani imekuwa ikiwasahau ukizingatia mchezo huo ni michezo
kama ulivyo mingine na kwamba mchezo huo umekuwa ukifundishwa pia
katika majeshi mbalimbali hapa nchini.
Hayo yamesemwa nakapteni wa timu na katibu msaidizi wa chama cha
Katrate mkoa wa Kilimanjaro bwana Wembo Hamisi katika viwanja vya
mazowezi mkoani hapo na amekusema kuwa wamekuwa wakikwama mara
wanapohitajika kwenye mechi za kirafiki,ndani na nje ya nchi kwasababu
hawana sapoti kutoka serikalini na wafadhili.
Aidha
amesema kuwa Karate ni mchezo ambao mtu yeyote anaweza kuucheza na
akatengeneza afya ya mwili,na mchezo huo ni wa kawaida kama ilivyo
michezo mingine kama mpira wa miguu amewataka watu wote kujitokeza kwa
wingi kujiunga katika mchezo huo wa Karate kwa sifa kuu ya karate ni
nidhamu.
Sambamba na hayo bwana Wembo amesema kuwa katika mchezo huo wapo
wanawake na ameiomba jamii waondokane na ile dhana potofu kwamba
mwanamke akicheza mchezo huo wa Karate hawezi kupata mtoto na kufanya
shughuli nyingine za kijamii amesema huo ni upotoshaji kwani mwanamke
anao uwezo wa kupata mtoto kama walivyo wengine na anatengeneza afaya
nzuri kabisa.
Aidha
amesesema kuwa mchezo huo wa Karate kwa historia umeanzishwa miaka
mingi kwa mkoa wa Kilimanjaro chama cha karate kina takribani miaka
saba sasa tangia kuanzishwa kwa chama hicho,na baadae wakaunda
shirikisho la Karate nchini Tanzania ambapo inajumuisha michezo yote ya
karate ,ambapo januari 30 watakuwa na tamasha la Karate la
kuwatambulisha wachezaji wa timu litakalofanyika mkoani hapo katika
ukumbi wa shule ya msingi Mwenge.
Katibu
huyo ameinisha ratiba yao ndani ya miezi sita ambapo watafanya
matamasha mbalimbali ikwemo februari 13/2016 watafanya tamasha wilayani
Same katika ukumbi wa kimweli same mjini, machi 24-26, mashindano
ya mchezo wa GOJUKAI KARATE ya Afrika Mashariki, Kampala Uganda ,
aprili 30 mashindano ya GOJUKAI Karate ya wazi ya kuuenzi mlima
Kilimanjaro ambapo watashiriki watoto wenye umri wa kati na watu
wazima yatafanyika Moshi.
Mwisho
ni Tamasha la shukrani litakalofanyika mei 16 hapo hapo Moshi
Kilimanjaro.
Kwa mkoa wa Kilimanjaro mchezo wa karate unaochezwa unajulikana kama
Gojukai Stayle, ambayo ilianzishwa kutoka nchini Japan,na chama katika
mkoa huo kinaundwa na vilabu mbalimbali ambavyo klabu mama ni Ralway
club, Pasua Club, Mwenge Club, Ccp Club,Rau Club,na vilabu vingine
vinaundwa na wanafunzi mbalimbali ambapo kila club ina zaidi ya
wanafunzi 20-30.hivyo wanawaomba ,Taasisi mbalimbali
,wafanyabiashara,makampuni mbalimbali hata watu binafsi kujitokeza
kuudhamini mchezo huo wa Karate.
JOCKTAN MALULI, DANIEL MSIRIKALE WAIBUKA WASHINDI KATIKA SHINDANO LA BONGO STYLE
Mshindi
wa Ubunifu mitindo Jocktan Cosmas Maluli A.k.a Makeke(aliyeshika cheti)
akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa shindano hilo kuanzia
kushoto ni Zamda George, Comfort Badaru, Martin Kadinda, Reuben Nabora
na Stanley Kamana.
Mshindi wa kipengele cha The Best Photographer, Daniel Msirikale (mwenye miwani) akipokea tuzo yake.
Mratibu wa FASDO nchini, Joyce Msigwa akitoa muhtasari wa shindano la Bongo Style.
Mshereheshaji, Mario Mpingirwa akifafanua jambo.
Mtumbuizaji wa ngoma za asili akionesha uwezo wake wa kuchezea nyoka.
SHARE









No comments:
Post a Comment