TRA

TRA

Tuesday, January 19, 2016

MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU LETICIA NYERERE

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Misa ya kumbukumbu ya marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki kutok kila kona ya Marekani. Mwili wa marehemu Leticia Nyerere unatarajia kufika Tanzania kesho Jumanne January 19, 2016 na utaagwa Dar es Salaam na mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Butiana. Picha na Iska Jojo.
Wana familia wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani. Kutoka kushoto ni Bi. Kijogoo kutoka Arizona,,Margareth Mageni na ,Flora Mageni
Wanafamilia wakiwemo watoto wa marehemu kutoka kushoto ni Julius Nyerere, Helena Nyerere na Julia Nyerere kulia ni Edlaila  Nyerere ambaye ni wifi wa marehemu kutoka Atlanta jimbo la Georgia nchini Marekani  wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya mpendwa mama yao Leticia Nyerere aliyeaga Dunia siku ya Jumapili January 10, 2016 katika hospitali ya Jumuiya ya Madaktari iliyopo Lanham, maryland nchini Marekani.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akitoa mkono wa pole kwa mume wa marehemu Madaraka Nyerere kwenye misa ya kumbukumbu  ya marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki

Balozi Wilson Masilingi akiongea machache na kutoa pole kwa wafiwa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger