MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Leticia
Nyerere (Chadema), umewasili Dar es Salaam leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
Julius Nyerere na utaagwa kesho Msasani.
Wakati mwili huo unawasili ndugu wa marehemu
walikuwa wamefika kwa wingi katika uwanja huo ambapo ulipokelewa na kisha
kuingizwa kwenye gari maalumu.
Mwili wa Leticia ulipelekwa moja kwa moja Kanisa Katoliki
la St.Peter's jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ibada maalumu na kisha
kupelekwa nyumbani kwake Msasani.
SHARE
No comments:
Post a Comment