Baadhi
ya Wananchi wa Mtaa wa Chira Kata ya Kenyamanyoro katika Halmashauri ya
Mji wa Tarime Mkoani Mara wakishiriki zoezi la ukarabati mdogo wa
barabara ya Muturu (Remaghinga) iliyopo Mtaa wa Buguti Kata ya Rebu
ambayo inayotegemewa na Wakazi Kata zote mbili za Kenyamanyori na Rebu
hatika halmashauri hiyo.
Zoezi
hilo limefanyika leo Januari 02,2016 ambapo wananchi hao walikuwa
wakifanya ukarabati wa kujaza moramu katika maeneo yaliyochimbika
kutokana na maji ya mvua pamoja na kuchimba mitaro kwa ajili ya
kupitisha maji wakati wa mvua.
“Hii
barabara ni kama imesahaulika na Halmashauri ingawaje ni mhimu sana
kwani tegemeo kwa wananchi pamoja na shughuli mbalimbali kama vile
ujenzi kwa kuwa hapo ng’ambo kuna shughuli za uchimbaji wa mawe hivyo
malori huwa yanapita hapa kwa ajili ya kwenda kufuata mawe hayo kwa
ajili ya ujenzi katika maeneo mbalimbali ya mji”. Alibainisha mmoja wa
wananchi hao na kuongeza kuwa imekuwa kawaida yao kufanya ukarabati wa
aina hiyo pindi barabara hiyo inapoharibika.
Hatua
ya Wananchi hao inapaswa kuigwa na wanajamii wengine pamoja na viongozi
wenye dhamana ya kuwasimamia katika masuala ya maendeleo wakiwemo
watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa kwani maendeleo yanapatikana
haraka zaidi ikiwa wanajamii watashiriki ipasavyo katika shughuli zao
za kimaendeleo badala ya kuishia kulalamika mitaani.
Na:George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group
Baadhi
ya Wananchi wa Mtaa wa Chira katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani
Mara wakishiriki zoezi la ukarabati mdogo wa barabara ya Muturu
(Remaghinga) inayotegemewa na Wakati Kata za Kenyamanyori na Rebu hatika
halmashauri hiyo.
Hii ndiyo dhana halisi ya Maendeleo
Wanajamii wajiwekee utaratibu wa kutatua kero mbalimbali za kimaendelo katika maeneo/mitaa yao
Wanajamii wajiwekee utaratibu wa kutatua kero mbalimbali za kimaendelo katika maeneo/mitaa yao
Maendeleo yanaanza na kila mmoja katika jamii
Kulalamika mitaani si suluhisho la utatuzi wa kero mbalimbali katika jamii
George Binagi-GB Pazzo ambae ni Mwanahabari na Mmiliki wa Mtandao wa Binagi Media Group (Mwenye jembe) nae alishiriki zoezi hilo
George Binagi-GB Pazzo ambae ni Mwanahabari na Mmiliki wa Mtandao wa Binagi Media Group (Mwenye jembe) nae alishiriki zoezi hilo
Barabara ya Muturu (Remaghinga) ni tegemeo kwa wananchi wa kila rika wakiwemo watoto
Hakika barabara hii imeharibika sana na inahitaji ushirikiano zaidi ili kuweza kurejea katika hali nzuri
Picha
hii inaonesha baadhi ya makazi ya watu wanaotegemea barabara hiyo ya
Muturu (Remaghinga) ambapo imepigwa kutoka ng’ambo ya pili inakoelekea
barabara hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment