Mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi akiasindikizwa na wafuasi wake mahakamani, Lubumbashi, Mei 11, 2016.
Wafuasi wa Moïse Katumbi mbele ya mahakama Mei 11, 2016.
Na RFI
Mwanasiasa
wa upinzani Moïse Katumbi, mgombea aliyejitangaza kuwania kiti cha
urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ameshtakiwa Alhamisi hii
Mei 19 kwa kosa la "kuhatarisha usalama wa ndani na nje ya nchi",
Mwendesha mashtaka mkuu wa Jamhuri mjini Kinshasa amesema.
Nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mashtaka yanakwenda sambamba na mwisho
wa hatua ya uchunguzi na mkuu wa zamani wa zamani wa mkoa wa Katanga
sasa anasubiri rasmi kesi kuanza.
Moïse
Katumbi anashtumiwa na serikali ya Congo kuajiri mamluki kwa lengo la
kuhatarisha usalama wa taifa, wiki kadhaa baada ya kuchukua uamuzi wa
kurasimisha kugombea kwake katika kiti cha urais katika uchaguzi
uliopangwa kufanyika mwaka huu.
Jumatano
Mei 4 Waziri wa sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, Alexis
Thambwe Mwamba alisema kwamba aliamuru uchunguzi kuhusu madai ya
"kuajiriwa kwa mamluki" wa kigeni yanayohusishwa mkuu wa zamani wa mkoa
wa Katanga (kusini), Moïse Katumbi.
"Ninatoa
amri kwa PGR (Mwendesha mashitaka mkuu wa Jamhuri) kuanzisha uchunguzi
katika mkoa wa zamani wa Katanga (...) Tuna nyaraka za ushahidi kuwa
askari kadhaa wa zamani wa Marekani ambao kwa sasa wako Katanga
wanafanya kazi kwa maslahi ya Bw. Katumbi , " Waziri wa Sheria wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Alexis Thambwe Mwamba, alisema katika
mkutano na waandishi wa habari.
"Mtego wa ujanja tena hatari"
"Utawala
unataka kunidhuru na mambo yote yako sawa. Nina imani na raia na
waangalizi wa kimataifa ambao hawaanguka katika mtego huu wa ujanja na
hatari ", Moïse Katumbi alitangaza wiki mbili zilizopita.
Katumbi
mwenye umri wa miaka 51 alijiunga na upinzani mwezi Septemba, baada ya
kujiuzulu kama mkuu wa mkoa wa Katanga (kusini)na aliondoka katika chama
cha urais. Bw Katumbi ni mmoja wawatu maarufu nchini Congo,
mfanyabiashara tajiri pia ni kiongozi wa kifahari wa klabu ya soka ya
Tout-Puissant Mazembe ya Lubumbashi, mshindi mara tatu wa Ligi ya
Mabingwa barani Afrika.
Hali ya
kisiasa imeendelea kuwa tete kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa
uwezekano mkubwa wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais ambao umepangwa
kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba. Upinzani anamtuhumu Kabila,
madarakani tangu mwaka 2001 na ambaye Katiba inampiga marufuku ya
kuwania katika uchaguzi huo.RFI(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment