TRA

TRA

Friday, May 20, 2016

MWINYI: BENKI ZA KISLAM ZINATOA MIKOPO BILA RIBA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 

1
RAIS Mstaafu wa awamu ya Pili,  Alhaj Dk. Ally Hassan Mwinyi akisoma hotuba yake wakati alipozindua kongamano la tatu la Taasisi za Kifedha za Kiislam Afrika, lenye lengo la  kujengeana uwezo na wadau  wa  sekta za kifedha kwa watendaji wa taasisi hizo linalofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency kwa siku mbili.
2
Baadhi ya wadau wakiwa katika Kongamano la tatu la Taasisi za Kifedha za Kiislam Afrika, lenye lengo la  kujengeana uwezo na wadau  wa  sekta za kifedha kwa watendaji wa taasisi hizo.
3
Baadhi ya wasiriki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
4
RAIS Mstaafu wa awamu ya Pili,  Alhaj Dk. Ally Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo.
RAIS Mstaafu wa awamu ya Pili,  Alhaj Dk. Ally Hassan Mwinyi, amesema kuwa  benki zimekuwa zikiendeshwa kwa kutoa  mkopo bila riba hivyo  itasaidia watanzania  kujiwekea akiba na  kuweza kukopa kwa ajili ya maendeleo yao .
Mwinyi a ameyasema hayo leo , wakati akifungua kongamano la tatu la Taasisi za Kifedha za Kiislam Afrika, lenye lengo la  kujengeana uwezo na wadau  wa  sekta za kifedha kwa watendaji linalofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency  kwa siku mbili katika  kuwezesha urahisishaji wa usimamizi wa taasisi hizo na fursa ambazo wanaweza kuwekeza katika nchi za Afrika ikiwemo na Tanzania.
Amesema zipo baadhi ya benki  zinatoza riba kubwa, hali inayowafanya wananchi  baadhi ya  wananchi  kujiunga taasisi za kifedha na  kuogopa kukopa mikopo kitokana na riba wanazotoza.
Aidha amewawahamasisha wananchi kujiunga na benki  za kiislaam  ili kujiwekea akiba na kukopa fedha bila riba.
Nae Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bima ya Kiislam Zanzibar, Said Abdallah, amesema asilimia 15  ya wananchi wanaojiunga na mfumo mpya wa bima ya Kiislam ni wapya.
“Kuna umuhimu ya kuanzisha bima nyingine za kiislam nchini katika  kuwezesha wananchi  kujiunga na bima kwa ajili ya maisha yao,”amesema Rais Mstaafu, Mwinyi.
Amesema pia sheria ya kuandaa bima za kiislam ni changamoto kubwa na kwamba hawajapata kibali  kwa kamishina wa Bima tangu wameanza kufuatilia mwaka 2008 .(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger