Obama akiweka shada ya maua Hiroshima.
Obama
amekuwa rais wa kwanza wa Marekani aliyeko madarakani kuzuru eneo la mji
wa Hiroshima ambalo Marekani ilishambulia kwa kutumia bomu la kwanza la
atomiki mwaka 1945 na kuua takriban watu 140,000.
Baada ya
kuweka shada ya maua katika bustani ya amani eneo la Hiroshima-Japan,
rais Obama alitoa hotuba ya kumbukumbu ya mashambulizi hayo ya Hiroshima
huku akisisitiza matumaini kuwa uhusiano kati ya Japan na Marekani
utazidisha matumaini katika juhudi za kutupilia mbali matumizi ya silaha
za atomiki.
Obama
amekuwa rais wa kwanza wa Marekani aliyeko madarakani kuzuru eneo la mji
wa Hiroshima ambalo Marekani ilishambulia kwa kutumia bomu la kwanza la
atomiki mwaka 1945 na kuua takriban watu 140,000. Obama amefanya ziara
hiyo ya kihistoria baada ya mkutano wa viongozi wa nchi saba tajiri
kiviwanda duniani ambapo viongzo hao wamekubali kuimarisha uchumi wa
dunia.
Upatanisho
Shambulizi
la bomu la kwanza la atomiki eneo la Hiroshima mwaka 1945 na pia
Nagasaki lilisababisha vifo maelfu ya watu papo hapo, na baadaye jumla
ya watu 140,000 walifariki. Japo hakuomba msamaha jinsi Ikulu ya White
House ilivyotangaza awali, Obama amesikitikia waliopoteza uhai wao miaka
71 iliyopita kufuatia mashambulizi hayo yaliyoifanya Japan kusalimu
amri na hivyo vita vikuu vya pili vikakamalizika.
Waziri
mkuu wa Japan Abe Shinzo ambaye ni mwenyeji wa Obama amesema, ziara ya
Obama katika bustani ya Hiroshima inafungua ukurasa mpya wa upatanisho
baina ya mataifa hayo mawili
Ziara ya
Obama inajiri wakati viongozi wa mataifa saba tajiri kiviwanda
wakikubaliana kuwa haja ya kuimarisha uchumi wa dunia inapaswa kupewa
kipaumbele ya dharura. Viongozi hao pia wameonya kuwa huenda kukatokea
athari kubwa ikiwa Uingereza itapiga kura ya kujiondoa katika Umoja wa
Ulaya, katika kura ya maamuzi inayotarajiwa mwezi ujao. Mkutano huo wa
siku mbili uliofanywa mji wa Ise-Shima Japan umekamilika. DW
SHARE








No comments:
Post a Comment