
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa kufungua Mafunzo ya siku tatu ya Wanawake
Wajasiriamali yalioandaliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF)
kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani, Dar es Salaam.(PICHA NA OMR).

Mwenyekiti
wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mhe. Mama Anna Mkapa akihutubia
kwenye ufunguzi wa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali ambapo mgeni
Rasmi wa ufunguzi huo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mtendaji
Mkuu wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Ndugu Steven Martin akielezea kwa
ufupi mafanikio ya mafunzo ambayo yametimiza miaka 19.

Sehemu
ya wakina ama waliohudhuria ufunguzi wa Mafunzo ya Wanawake
Wajasiriamali kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani,Dar Es Salaam.

Mjumbe
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Esther
Mkwizu akizungumza na wajumbe walihudhuria mara baada ya unfunguzi rasmi
wa mafunzo kufanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la JKT Mgulani jijini Dar
es Salaam.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mama Janetth Magufuli ,Mkuu wa Wilaya ya Temeke
Mhe. Sophia Mjema wakifurahia jambo wakati wa shughuli za ufunguzi wa
mafunzo ya wajasiriamali wanawake ,kushoto ni Mwenyekiti wa wa Mfuko wa
Fursa Sawa kwa Wote, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mama Anna
Mkapa.

Baadhi ya wakina Mama waliohudhuria wakifuatilia kwa makini hotuba za ufunguzi wa mafunzo ya wanawake wajasiriamali.

Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Bi.Jacline
Maleko akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan pamoja na Mwenyekiti wa Mfuko wa
Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo
kwa Wanawake Wajasiriamali yaliofanyika kwenye Bwalo la JKT Mgulani
jijini Dar es Salaam.
SHARE








No comments:
Post a Comment