Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga, Moïse Katumbi,wakati akihojiwa Lubumbashi, Juni 2, 2015.
Afisa wa
mashitaka ameombea hukumu ya kifungo cha miaka mitano jela dhidi ya
Moise Katumbi, Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga. Anatuhumiwa
kupokonya na kuuza nyumba ya Bw Alexandros Stoupis, raia wa Ugiriki.
Kesi hii ilisikilizwa, Jumatatu, Juni 20, katika mahakama ya mjini Lubumbashi (Haut-Katanga).
Wanasheria
wa Moise Katumbi, waliokuwepo wakati wa kesi hiyo, hawakuruhusiwa
kuwakilisha mteja wao, ambaye yupo kwa wiki tatu Ulaya kwa ajili ya
matibabu.
Mahakama
imetoa hoja kwamba wakati mtuhumiwa anakabiliwa na kosa, ambalo adhabu
yake ni zaidi ya miaka mitano, kuripoti kwake mahakamani kunahitajika.
Kutokana na kutokuwepo kwa Moise Katumbi, mahakama ilianza na kufunga uchunguzi wa kesi.
Upande wa
mashtaka waliomba adhabu ya kifungo cha miaka 5 dhidi ya Moise Katumbi,
wakati ambapo hukumu rasmi inatarajiwa ndani ya muda wa siku nane.
Mashitaka
hayo yamekua mwezi mmoja baada ya mgombea kutangaza kuwania kiti cha
urais katika uchaguzi wa urais unaopangwa kufanyika mwaka huu. Awali
alishitakiwa kwa kosa la "kuhatarisha usalama wa taifa" na kuwekwa chini
ya kibali cha kukamatwa kwa muda. Kibali hiki kilitokewa na Mwendesha
Mashtaka Mkuu wa Jamhuri.
Katika kesi hiyo, alishtakiwa kuajiri mamluki wa kigeni kwa lengo la kuhatarisha usalama wa taifa.
Pamoja na hukumu hiyo, Moise Katumbi alipa ruhusa kutoka kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Jamhuri kufanyiwa matibabu nje ya nchi.
Mkuuwa
zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga alisafirishwa tarehe 20 Mei nchini
Afrika Kusini kwa matibabu. Moise Katumbi aliondoka Afrika Kusini Mei 28
akielekea Ulaya kuendelea kupata matibabu. RFI
SHARE








No comments:
Post a Comment