Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Gideon
Manambo akizungumza na watumishi wa Wizara (hawapo pichani) katika
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Ukumbi wa
Wizara hiyo. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Doto
James.
Baadhi ya
Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifurahia jambo wakati
Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Bw. Doto
James akifafanua hoja mbalimbali za watumishi.
Watumishi
wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa wamesimama kwa dakika chache
kuwakumbuka watumishi waliotangulia mbele za haki kwa mwaka huu, katika
mkutano huo.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakibadilishana mawazo baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
Picha ya pamoja.
Wizara ya
Fedha na Mipango imeadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya
mkutano na Watumishi wake, lengo likiwa ni kujadili mafanikio na
changamoto wanazo kabiliana nazo mahali pa kazi.
Akizungumza
wakati wa maadhimisho hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James aliwataka Watumishi kuunga mkono juhudi za
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Magufuli
katika kupambana na masuala ya rushwa, uzembe kazini na Watumishi hewa
ambao wamekuwa wakiigharimu Serikali fedha nyingi katika kutekeleza
majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Alisema
Wizara inajipanga kuhakikisha inaboresha mazingira ya kazi kwa watumishi
hasa kwa wale wenye ulemavu kwa kuwajengea miundombinu rafiki sehemu
za kazi ili kuongeza ufanisi kazini.
“Wizara
pia inafanya vizuri katika masuala ya usawa wa kijinsia kwa kuwa na
idadi inayoridhisha ya wanawake hasa katika ngazi za maamuzi, ikiwa ni
pamoja na kuwa na Manaibu Katibu Wakuu wawili wanawake” . Alisisitiza
James
Naye
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango,
Bw. Gideon Manambo alisema kuwa, watumishi wanatakiwa kufanya kazi kwa
ufanisi na kwa bidii ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya maendeleo
ambayo yanahitaji watendaji wenye weledi wa kutosha ili kukabiliana na
changamoto zinazojitokeza.
Kwa
upande wa watumishi wa Wizara, wameuomba uongozi kuhakikisha kunakuwepo
na vitendea kazi vya kutosha ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa
na matokeo chanya ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayowakabili
wananchi.
Maadhimisho
hayo yamefanyika kufuatia utaratibu mpya uliowekwa na Serikali ya Awamu
ya Tano ambapo uliagiza Wizara pamoja na Taasisi kuadhimisha Wiki hiyo
kwa kutatua matatizo ya watumishi wa Umma pamoja na wananchi kwa ujumla
katika maeneo yao ya kazi.
Imetolewa na: Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango. (P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment