Mkurugenzi
wa Mradi wa PS3 Dk. Emmanuel Malangalila akizungumza wakati wa ufunguzi
wa mafunzo ya siku mbili yaliyo wakutanisha pamoja wataalam mbalimbali
wanaohusika na usimamizi wa rasilimali watu kutoka katika mikoa na
tasisi za serikali ili kupata kitini cha kutolea mafunzo kwa watumishi
wapya wanaoajiriwa serikalini. Mafunzo hayo yanafanyika mjini Bagamoyo
mkoani Pwani.
Mafunzo
hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya
Sekta za Umma (PS3) nchini ambao unatekelezwa katika mikoa 13 na
kuzinufaisha halmashauri 97.
Baadhi ya maofisa kutoka Ofisi ya Rais, tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Serikali za Mitaa, Miriam Mmbaga akifuatiwa na Beatice Kimoleta
Washiriki
wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa rasilimali watu
katika taasisi na Halamashauri mbalimbali nchini. Mafunzo hayo yanalenga
kuwaweza waajiri hao kutafuta mbinu ikiwepo mafunzo na motisha
mbalimbali kwaajili ya kuwafanya watumishi wapya wanapoajiriwa kuendelea
kufanya kazi katika mazingira yeyote.
Mkuu
wa Kitengo cha Mifumo ya Rasilimali wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo
ya Sekta za Umma (PS3) Josephine Kimaro akitoa mafunzo kwa viongozi wa
sekta ya Afya waliojitokeza kushiriki semina hiyo mjini Bagamoyo mkoani
Pwani.
Washiriki
wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa rasilimali watu
katika taasisi na Halamashauri mbalimbali nchini. Mafunzo hayo yanalenga
kuwaweza waajiri hao kutafuta mbinu ikiwepo mafunzo na motisha
mbalimbali kwaajili ya kuwafanya watumishi wapya wanapoajiriwa kuendelea
kufanya kazi katika mazingira yeyote. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment