Mwenyekiti
wa KIFIDA aliyemaliza muda wake, Hassan Ngubege akimkabidhi Mwenyekiti
mpya wa chama hicho Jesse John katiba ya chama hicho.
Na Mwandishi Wetu,Kisarawe
MTANGAZAJI
nguli wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jesse John amechaguliwa
kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kisarawe (KIDIFA)
katika uchaguzi uliofanyika jana.
Jesse
ambaye aliupata uongozi huo katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa
aliibuka kidedea baada ya kupata kura 32 na kumshinda mpinzani wake
Karim Wenge aliyepata kura 21.
Katika
uchaguzi huo Mohamed Lubondo alichaguliwa kuwa Katibu baada ya kupata
kura 30 na kumshinda Francis Mkamba aliyepata kura 27.Katibu Msaidizi
alichaguliwa kuwa Amosi Kisebengo, Makamu Mwenyekiti alichaguliwa kuwa
Abdul Mogella.
Wasimamizi
wa uchaguzi huo kutoka Chama Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA),
Mweka Hazina wa KIDIFA alichaguliwa Iddo Mtangaze na Mweka Hazina
Msaidizi alichaguliwa kuwa Sadiki Nasoro.
Mwakilishi
wa klabu kutoka Tarafa ya Mzenga alichaguliwa kuwa Suleiman Mahenge,
kutoka Tarafa ya Sungwi alichaguliwa Abdallah Kuga na Mwakilishi wa
klabu alichaguliwa kuwa Ally Madega na Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa
mkoa alichaguliwa kuwa Mohamed Masenga.
Mwenyekiti
wa KIDIFA aliyemaliza muda wake Hassan Ngubege akimkarisha Jesse
kushukuru wajumbe aliwataka viongozi wapya kufufua matumaini ya vipaji
vya vijana katika soka wilaya ya Kisarawe kwa kuanzisha mashindano
mbalimbali yenye lengo la kutafuta vipaji.
Jesse
akiwashukuru wajumbe hao aliahidi kushirikiana na wadau wa soka ndani na
nje ya wilaya hiyo kupata timu ya wilaya itakayoshiriki Ligi Kuu ya
Vodacom kama timu nyingine zinashiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti
Jesse alisema wilaya ya Kisarawe ambako yeye ni mzaliwa wa asili
alisema anaamini vijana wengi hawajapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao
hivyo atatumia miaka minne ya uongozi kuzalisha vijana wazuri katika
soka. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment