Kaimu
Katibu Tawala mkoani Mwanza, Projestus Rubanzibwa, akizungumza kwa
niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, kwenye kikao cha Utambulisho wa Mradi
wa kuongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini katika
mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi, kilichofanyika hii leo
Jijini Mwanza.
Amesisitiza
kwamba Wakuu wa Vyuo vya vya Ukunga nchini wanao wajibu wa kuhakikisha
kwamba wanatoa mafunzo bora kwa wahitimu wa vyuo hivyo ili
watakapohitimu masomo yao waweze kusaidia kutoa huduma bora afya.
Mradi
wa kuongeza Ujuzi na Idadi ya Wakunga katika maeneo ya Vijijini,
unatekelezwa na Shirika la Jhpiego kwa kushirikiana na Taasisi ya
Wakunga nchini Canada, Shirika la Amref, Serikari ya Canada, Taasisi ya
Wakunga Tanzania na Wizara ya Afya nchini, lengo likiwa ni kuboresha
huduma za afya kwa akina mama na mtoto ili kutokomeza vifo vitokanavyo
na uzazi maeneo ya Vijijini nchini.
Na BMG
Kaimu
Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, Dr.Silas Wambura, akizungumza kwa niaba ya
Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza, ambapo amesema mkoa wa Mwanza unakabiriwa na
upungufu mkubwa wa idadi wa wakunga pamoja na vifaa tiba hali ambayo
inasababisha kuwepo kwa vifo vya akina mama na watoto.
Dr.Dustan
Bishanga ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Mama na Mtoto Shirika la
Jhpiego, amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha unaongeza Ujuzi na
Idadi ya Wakunga maeneo ya Vijijini hapa nchini ambapo wahitimu wa
masomo ya Sayansi katika maeneo hayo watakuwa wakipewa ufadhiri wa
masomo kwa makubaliano ya kurudi kwenye maeneo yao ili kutoa huduma za
afya. Mradi huo unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2021.
Kikao
cha Utambulisho wa Mradi wa kuongeza ujuzi na idadi ya Wakunga katika
maeneo ya Vijijini mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi
kilichofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Dr.Dustan
Bishanga ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Mama na Mtoto Shirika la
Jhpiego, akizungumza na wanahabari kwenye kikao hicho.
Martha
Rimoy ambaye ni Mratibu wa Taifa wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA),
amesema bado maeneo mengi nchini yanakabiloiwa na upungufu wa Wakunga
kutokana na idadi ya Wakunga wanaohitimu vyuoni kutoendana na idadi ya
ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya huku wengine pia wakishindwa kwenda
kufanya kazi maeneo ya Vijijini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
mazingira duni.
Gustav
Moyo ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga, Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, amesema hali ya
upungufu wa Wakunga nchini hususani maeneo ya Vijijini si nzuri hivyo
Serikali inatumia jitihada mbalimbali ikiwemo kuhamasisha wanafunzi
kusoma masomo ya Sayansi ili kutatua changamoto hiyo.
Amesema
asilimia kubwa ya mikoa ya Kanda ya Ziwa inakabiliwa na upungufu huo na
kwamba Serikali itakuwa ikitolea kipaumbele kwenye mikoa hiyo pindi
inapotoa ajira kwa Wakunga.
Kikao
hicho kimewajumuisha wadau mbalimbali wa afya wakiwemo Wakunga, Waganga
Wakuu wa Wilaya na Maafisa Elimu ambao watakuwa na wajibu wa
kuwahamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi ili kuongeza idadi ya
Wakunga.
Wadau wa afya kutoka Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Tabora, Kigoma na Mara wameshiriki kwenye kikao hicho.
SHARE
No comments:
Post a Comment