Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akielezea siku ya
kisomo duniani na dhumuni la UNESCO kuanzisha siku hiyo.
Kaimu
Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw.
Nicholaus Bureta akizungumzia juhudi za serikali za kuhakikisha kila
mtanzania anajua kusoma.
Mkurugenzi
Msaidizi Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, Basilina
Levira akitoa taarifa jinsi hali ilivyo kwa watu wazima ambao wanajua
kusoma na wasiojua kusoma.
Afisa
Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo akielezea mradi wa XPRIZE ambao
unasimamiwa na UNESCO ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa
kutumia uwezo walionao watoto katika maeneo mbalimbali nchi
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akitoa maelezo
kuhusu Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM).
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akimkabidhi mgeni
rasmi, Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta, Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani
2016 (GEM)
Mgeni
rasmi, Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta akionyesha Ripoti ya Ufuatiliaji wa
Elimu Duniani 2016 (GEM) baada ya kuipokea kutoka kwa Mkuu wa Ofisi na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez
Wageni
waalikwa katika maadhimisho ya siku ya kisomo duniani wakionyesha
Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM) wakiongozwa na Mkuu wa
Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez (wa kwanza kushoto).
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodriguez akimkabidhi mgeni
rasmi, Kaimu Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta, sanduku la Ripoti ya Ufuatiliaji wa
Elimu Duniani 2016 (GEM).
Mgeni
Rasmi katika maadhimisho ya siku ya kisomo, Kaimu Kamishna wa Elimu
kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta
akigawa Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu Duniani 2016 (GEM) kwa baadhi ya
wafanyakazi wa wizara yake.
Na Mwandishi wetu
Katika
kutambua umuhimu wa kusoma na kuandika Tanzania na mataifa mengine
duniani zimeungana kwa pamoja kuadhimisha siku ya Kisomo Duniani ambayo
huadhimishwa kila Septemba, 8 ya kila mwaka ambapo pamoja na maadhimisho
hayo pia iliambatana na Uzinduzi wa Ripoti ya Ufuatiliaji wa Elimu
Duniani (GEM).
Akizungumza
katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi.
Zulmira Rodriguez alisema kuwa dhumuni la UNESCO kuweka siku hii ya
Septemba 8 kila mwaka kuwa siku ya kisomo kimataifa ili kuziunganisha
jamii zote za kimataifa duniani kuweka na kuendeleza nguvu na juhudi kwa
watu kujua kusoma na kuandika ili kuleta maendeleo katika jamii
mbalimbali.
“Kauli
mbiu hii inatufungulia milango ya uelewa juu ya malengo na mafanikio ya
miongo mitano iliyopita ambayo yaliwekwa ya kutaka kila mtu anajua
kusoma,” alisema Bi. Rodrieguez na kuongeza.
“Tunataka
kujua ni changamoto gani zinazoikabili sekta ya elimu katika kusoma na
kuandika na tunataka kufahamu namna ya kukabiliana na changamoto hizo
ili kufikia malengo ambayo UNESCO iliyakusudia kufikiwa ya kila mmoja
awe anajua kusoma.”
Kwa
upande wa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Kaimu Kamishna wa Elimu
kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Nicholaus Bureta
ambaye alimuwakilisha Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo alisema
serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imejizatiti
kuondoa tabaka la wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa vijana na
watu wazima kwa kujenga uwiano sawa wa utoaji wa elimu kwa watu wote.
“Wizara
imejipanga vizuri, na lengo kubwa la wizara ni kuhakikisha tunakuwa na
mtanzania aliye elimika na aliye na stadi, maarifa na uwezo wa kutumia
elimu aliyoipata,” alifafanua Bureta.
Vile
vile Bw. Bureta amesema kwa sasa wizara ipo kwenye mpango wa kukuza
stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) ambao unaanzia chini kwa
wanafunzi wa awali mpaka shule za msingi.
Katika
mpango huo walimu wamekuwa wakipata mafunzo mbalimbali ya namna ya
kumuwezesha mwanafunzi kujua Kusoma Kuandika na Kuhesabu katika ngazi ya
elimu ya awali.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya
Mfumo Rasmi, Basilina Levira amesema kwamba kwa mujibu wa sensa ya mwaka
2012, asilimia 78 ya vijana na watu wazima ndio waliokuwa wakijua
kusoma na kuandika.
Akaongeza
kuwa mwaka 2015 idadi hiyo ya wanaojua kusoma na kuandika ilishuka na
kufikia asilimia 77 ambapo ilipelekea wizara hiyo kutoka na mikakati
inayokusudia kuondoa kabisa tabaka la watu wasiojua kusoma na kuandika
nchini.
Aidha,
Basilina amesema kuwa Serikali ilipitisha sheria ya vyumba vya madarasa
ya shule zote nchini kutumika kufundishia vijana na watu wazima ambao
hawajui kusoma na kuandika muda wa jioni baada ya wanafunzi wa kawaida
wanapomaliza masomo yao.
Amefafanua
kwa kusema kuwa, wizara imeandaa programu ambayo iko kwenye mfumo wa
Televisheni na picha za video (DVD) yenye masomo 65 ya kujifunza kusoma,
kuandika na kuhesabu, ambapo kwa kutumia programu hiyo mwanafunzi
anaweza kujua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa muda wa miezi 4 mpaka 6.
Mafunzo
hayo kwa njia ya Televisheni na Picha za Video tayari yameanza kutumika
kwa wilaya za Ilemela, Dodoma Manispaa, Songea Manispaa, Bagamoyo,
Mkuranga, Temeke, Ilala na Kinondoni, ambapo asilimia 65 ya vijana na
watu wazima wasiojua kusoma na kuandika wamejitokeza kujiunga na Elimu
hiyo huku idadi kubwa ikiwa ni ya wanawake.
Siku
ya Kisomo Duniani huadhimishwa Duniani kote kila ifikapo Septemba, 8 ya
kila ya mwaka, ambapo mwaka huu 2016 maadhimisho hayo yametimiza miaka
50 tangu yalipoanza kuadhimishwa mwaka 1966.
Kauli
mbiu ya siku ya kisomo duniani kwa mwaka huu ni ‘Tunasoma yaliyopita,
Tunaandika yajayo, Elimu endelevu’ ambayo kwa lugha ya kiingereza ni
‘Reading the future, Writing the past’.
SHARE
No comments:
Post a Comment